Imepokelewa Kutoka kwa Jundub -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kabla ya kufariki kwake kwa sik...
Alinieleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, nakuwa nafasi yake imefikia kiwango cha juu kabisa cha m...
Kutoka kwa Abul Hayyaji A-Asady amesema: Ally bin Abii Twalib alisema kuniambia: Hivi sikutumi katika yale aliyonituma kwayo Mtume -Rehema na amani zi...
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwatuma Masahaba wake wasiache "Sanamu" nayo ni picha ya kiumbe hai yenye kiwiliwili- isipokuwa wameli...
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kuamini mikosi ni shirki, Kua...
Ametahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutokana na imani ya mikosi: Nayo ni kuamini mikosi ya chochote chenye kusikika au chenye kuonek...
Imepokewa kutoka kwa Imran bin Huswain - Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Si miongoni mw...
Katoa onyo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa atakayefanya baadhi ya matendo katika umma wake kwa kauli yake: "Si miongoni mwetu" Miongoni mway...
Kutoka kwa Anasi Bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna kuambukizana maradhi, wal...
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kuambukizana ambako walikuwa wakiamini watu wa zama za ujinga kuwa maradhi yanahama yenyewe kwenda...
Imepokelewa Kutoka kwa Jundub -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kabla ya kufariki kwake kwa siku tano naye akisema: "Hakika mimi ninajivua dhima kwa Mwenyezi Mungu, kwa mimi kuwa na mwandani (Mtu mwenye mapenzi ya dhati zaidi) miongoni mwenu, hakika Allah Mtukufu kanifanya mimi kuwa mwandani wake, kama alivyomfanya Ibrahim kuwa mwandani, na lau kama ningelijifanyia mwandani katika umma wangu basi ningemfanya Abubakari kuwa mwandani, tambueni kuwa; Hakika wale waliokuwa kabla yenu walikuwa wakiyafanya makaburi ya Manabii wao na wema wao kuwa misikiti, tambueni vyema (kuweni makini)! yakuwa Msijelifanya kaburi langu kuwa msikiti, hakika nakukatazeni msifanye hilo".
Kutoka kwa Abul Hayyaji A-Asady amesema: Ally bin Abii Twalib alisema kuniambia: Hivi sikutumi katika yale aliyonituma kwayo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-? (Nenda) Kamwe usiache sanamu au picha ila uifute, wala kaburi refu kupita kiasi isipokuwa umelisawazisha.
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kuamini mikosi ni shirki, Kuamini mikosi ni shirki, Kuamini mikosi ni shirki, alisema hivyo mara tatu", Na hakuna yeyote miongoni mwetu isipokuwa ana chembe ya hilo, isipokuwa Mwenyezi Mungu huliondoa kwa kumtegemea.
Imepokewa kutoka kwa Imran bin Huswain - Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Si miongoni mwetu atakayetafuta kujua habari za mikosi au akafanyiwa, au akafanya ukuhani au akafanyiwa, au akaroga au akarogewa, na atakayefunga fundo lolote, na atakayemuendea kuhani na akamsadikisha kwa yale ayasemayo atakuwa amekufuru yale yaliyoteremshwa kwa Muhammadi Rehema na amani ziwe juu yake".
Kutoka kwa Anasi Bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna kuambukizana maradhi, wala kutuhumu mikosi kwa sababu ya ndege, na kinachonipendeza zaidi ni kujipa matumaini". Wakasema: Ni nini matumaini? Akasema: "Ni neno jema".
Imepokelewa kutoka kwa Zaid Bin Khalid Aljuhaniy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alitusalisha Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- Sala ya Asubuhi katika mji wa Hudaibiyah wakati mvua iliponyesha usiku, na alipomaliza akawageukia watu na kuwauliza: "Hivi mnajua kuwa Mola wenu amesema nini?" Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanajua zaidi, akasema: "Watu wangu kwenye kuteremka Mvua wamegawanyika makundi mawili kuna waumini na makafiri, Basi yeyote atakayesema tumenyeshelezewa Mvua kwa fadhila za Mwenyezi Mungu basi huyo ni mwenye kuniamini mimi, na ni mwenye kuupinga unajimu, ama atakayesema kuwa tumenyeshelezewa Mvua kwa sababu ya nyota fulani na fulani, basi huyo amenikadhibisha mimi na kaziamini nyota."
Kutoka kwa Ukba Bin Aamir Al Juhaniy -Radhi za Allah ziwe juu yake: Yakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake lilikuja kwake kundi, akawaunga mkono watu tisa na akamuacha mmoja, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, umewaunga mkono watu tisa na ukamuacha huyu? akasema: "Huyo yuko na hirizi", akaingiza mkono wake akaikata, akamuunga mkono, akasema: "Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya ushirikina"
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika makombe, na hirizi, na limbwata, ni ushirikina".
Kutoka kwa baadhi ya wake za Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayemuendea mpiga ramli akamuuliza kuhusu lolote hazitokubaliwa sala zake siku arobaini".
Imepokelewa Kutoka kwa bin Omar -Radhi za Allah ziwe juu yao- yakwamba yeye alimsikia mtu mmoja akisema: Hapana! naiapia Al-ka'aba, akasema bin Omar: Hakuapiwi kinyume na Mwenyezi Mungu, kwani mimi nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atayeapa kinyume na Mwenyezi Mungu basi atakuwa amekufuru au kafanya ushirikina"
Kutoka kwa Buraida -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Atakayeiapia amana basi huyo si miongoni mwetu".
Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ary radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake nikiwa na kundi la Ash’ari ili kumuomba atuchukue, akasema: “Wallahi sitokuwa na chochote cha kukubebeni ” Kisha tukakaa muda kidogo aliopenda Mwenyezi Mungu tukae, tukaletewa ngamia, akaamrisha tupewe wanyama watatu kwa ajili yetu, tulipoondoka wakasema baadhi yetu kuwaambia wengine: Mwenyezi Mungu hatotubariki, tumemuendea Mtume rehema na amani ziwe juu yake tukamuomba atubebe katika vipando lakini akaapa kuwa hatotubeba, kisha akatubeba, akasema Abuu Musa: Basi tukaja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake tukamueleza hilo, akasema: “Si mimi niliyekubebeni, bali Mwenyezi Mungu ndiye aliyekubebeni Wallahi – akipenda Mwenyezi Mungu - sitokula kiapo cha jambo fulani isipokuwa ninapoona kilichobora zaidi basi huwa ninatoa kafara ya kiapo changu kisha ninafanya lililo bora zaidi.”