Imepokewa Kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msiseme: Ni kwakutaka Mwenyezi M...
Amekataza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kwa muislamu kusema katika maneno yake: "Akitaka Mwenyezi Mungu na akitaka fulani", Au akitaka Mwenyezi...
Imepokelewa kutoka kwa Mahmud bin Labid -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika ninachok...
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa jambo kubwa zaidi analoliogopea juu ya umma wake: Ni shirki ndogo nayo; ni mtu kufanya kwa ajili...
Kutoka kwa Abuu Dharri radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hatomtuhumu mtu mwenzake kwa...
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema kumwambia mwingine: Wewe ni muovu, au: Wewe ni kafiri, ikiwa hatokuwa kama alivyo...
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mambo mawili kwa watu hayo kwao ni ukafiri...
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mambo mawili kwa watu kuwa ni katika matendo ya makafiri, na ni tabia za enzi za ujinga, nayo ni:...
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Marthad Al-Anawiy -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msikae juu ya maka...
Amekataza -Rehema na amani ziwe juu yake- kukaa juu ya makaburi. Kama alivyokataza kusali kwa kuyaelekea makaburi, kwa kaburi kuwa upande wa kibla...

Imepokewa Kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msiseme: Ni kwakutaka Mwenyezi Mungu na fulani, lakini semeni: Akitaka Mwenyezi Mungu kisha akataka fulani".

Imepokelewa kutoka kwa Mahmud bin Labid -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika ninachokiogopea zaidi juu yenu ni shirki ndogo" Wakasema: Ni ipi shirki ndogo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni riyaa (kujionyesha), atasema Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya Kiyama kuwaambia, pindi watu wote watakapolipwa kwa matendo yao: 'Nendeni kwa wale mliokuwa mkijionyesha kwao duniani, mtazame je mtapata kwao malipo?".

Kutoka kwa Abuu Dharri radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hatomtuhumu mtu mwenzake kwa machafu, na wala hatomtuhumu kwa ukafiri, isipokuwa hurejea kwake, ikiwa ndugu yake hatokuwa hivyo".

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mambo mawili kwa watu hayo kwao ni ukafiri: Kutiana doa katika nasaba (ukoo), na kulia kwa kumuomboleza maiti".

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Marthad Al-Anawiy -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msikae juu ya makaburi, na wala msisali kwa kuyaelekea".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hawaingii Malaika nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha"

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hawafuatani Malaika na jamaa ambao ndani yao kuna mbwa au kengele".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: Shetani humjia mmoja wenu na akamwambia: Ni nani aliumba kitu fulani? Mpaka anafikia kusema ni nani alimuumba Mola wako? Basi ikiwa atafikia kuuliza hivyo basi na ajikinge kwa Mwenyezi Mungu na awache kuuliza maswali hayo."

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Hakika Mwenyezi Mungu amesema: Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi nitakuwa nimemtangazia vita, na hatojiweka karibu kwangu mja kwa kitu ninachokipenda katika vile nilivyomfaradhishia juu yake, na akawa bado mja wangu anaendelea kujiweka karibu yangu kwa ibada za sunna (zisizokuwa za lazima) mpaka nitafikia mahala nitampenda, nikishampenda: Nitakuwa sikio lake analosikilizia, na jicho lake analotazamia, na mkono wake anaoshikia, na mguu wake anaotembelea, na hata akiniomba hakika nitampa, na hata akinitaka kinga hakika nitamlinda, na sijawahi kusita katika jambo lolote ninalotaka kulifanya kama kusita kwangu katika (kuitoa) nafsi ya muumini, hapendi kufa na mimi sipendi kumuudhi".

Na kutoka kwa Irbadhi bin Sariya -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Siku moja alisimama kwetu sisi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akatupa mawaidha makali mno, nyoyo zilisisimka kwayo, na macho yalibugujikwa machozi, pakasemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Umetuwaidhi mawaidha ya mwenye kuaga, tuachie usia. Akasema: " Shikamaneni na kumcha Mwenyezi Mungu, na usikivu na utii, hata kama (mzungumzaji) atakuwa mtumwa tena muhabeshi (Muethiopia), na mtakuja kuona baada yangu hitilafu nyingi, basi shikamaneni na Sunna zangu na Sunna za makhalifa (watawala) waongofu, zing'ateni (mzikamatilie) kwa magego, na tahadharini sana na mambo ya kuzushwa, kwani kila uzushi ni upotevu".

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayejitoa katika utiifu, na akasambaratisha umoja akafa, atakuwa amekufa kifo cha zama za ujinga, na atakayepigana chini ya bendera kibubusa anachukia kwa sababu ya ndugu zake, au akahamasisha katika (kupendelea kwa sababu ya) udugu, au ana nusuru udugu, akauwawa, basi hicho ni kifo cha zama za ujinga, na atakayejitoa katika umma wangu, akimpiga mwema wake na muovu wake, na wala hajali muumini wake, na wala hamtimizii mwenye ahadi ahadi yake, basi huyo si miongoni mwangu na mimi si miongoni mwake".

Kutoka kwa Ma'akali bin Yasaari -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Hakika mimi nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakuna mja yeyote atakayepewa usimamizi na Mwenyezi Mungu kwa raia, akafa siku atakayokufa hali yakuwa aliwafanyia udanganyifu raia wake, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamharamishia pepo".