- Uharamu wa kusema: " Akitaka Mwenyezi Mungu na ukitaka", na mfano wa matamshi kama haya ambayo yatamaanisha kuunganisha neno na Mwenyezi Mungu kwa kiunganishi "Na"; kwa sababu hii ni katika shirki ya matamshi.
- Inafaa kusema: " Akitaka Mwenyezi Mungu kisha ukitaka", na mfano wa hayo ambayo yanamaanisha kuunganisha maneno kwa kiunganishi "Kisha"; kwa kuwa hakuna katazo ndani yake.
- Hapa kumethibitishwa matashi kwa Mwenyezi Mungu, na matashi ya mja, nakuwa matashi ya mja yanafuata matashi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Katazo la kuwashirikisha viumbe katika matashi ya Mwenyezi Mungu hata kama ni kwa matamshi.
- Ikiwa mtu ataitakidi kuwa matashi ya mja ni sawa na matashi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuenea kwake na kutokuwa na mipaka, nakuwa mja ana matashi binafsi ya kwake mwenyewe, hii ni shirki kubwa, ama akiitakidi kuwa matashi ya mja yanakaribia matashi ya Mwenyezi Mungu; hii ni shirki ndogo.