Imepokewa kutoka kwa Abdullahi Bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ni dhamb...
Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu dhambi kubwa akasema: Kubwa zaidi ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, nako ni kumuwekea Mwenyezi M...
Imepolelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Amesema Allah aliyetakasi...
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka amesema kuwa: Yeye amejitosheleza na uhitaji wa washirik...
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Umma wangu wote wataingia pe...
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba umma wake wote wataingia peponi isipokuwa atakaye kataa!. Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu...
Imepokelewa Kutoka kwa Omar bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Msichupe m...
Anakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kupitiliza na kuvuka mpaka wa kisheria katika kumsifu, na kumsifu kwa sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu n...
Imepokewa kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hawezi kua na imani mmoj...
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa muislamu hawezi kua na imani kamili mpaka atangulize mapenzi ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu...

Imepokewa kutoka kwa Abdullahi Bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ni dhambi ipi kubwa zaidi mbele ya Allah? Akasema: "Ni wewe kumuwekea Mwenyezi Mungu mshirika, na hali yeye ndiye aliyekuumba" Nikasema: Hakika hilo ni jambo kubwa, nikasema: Kisha ipi? Akasema: "Na kumuua mwanao; ukiogopea atakula pamoja nawe" Nikasema: Kisha ipi? Akasema: "Ni wewe kumzini mke wa jirani yako".

Imepolelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Amesema Allah aliyetakasika na kutukuka: Mimi nimetosheka (sihitaji) washirika kushirikishwa nao, yeyote mwenye kufanya jambo akashirikisha ndani yake mwingine pamoja nami, nitamuacha na ushirika wake".

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Umma wangu wote wataingia peponi isipokuwa atakaye kataa" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na ni nani atakaye kataa? Akasema: "Atakaye nitii ataingia peponi, na atakaye niasi atakuwa amekataa".

Imepokelewa Kutoka kwa Omar bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Msichupe mipaka katika kunisifu, kama walivyochupa mipaka Wakristo kwa mwana wa Mariam; Bila shaka, mimi ni mja wake, na semeni: Mja wa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake".

Imepokewa kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hawezi kua na imani mmoja wenu mpaka nipendeke kwake kuliko wazazi wake na mwanaye na watu wote".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Niacheni na vile nilivyo kuachieni, hakika waliangamia waliokuwa kabla yenu kwa sababu ya maswali mengi na kuwapinga mitume wao, hivyo, nikiwakatazeni jambo basi liepukeni, na nikiwaamrisha jambo lifanyeni kadiri muwezavyo"

Imepokelewa Kutoka kwa Abdallah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Fikisheni kutoka kwangu japokuwa aya moja, na simulieni kuhusu wana wa Israeli wala hakuna ubaya, na yeyote atakayenisemea uongo mimi kwa makusudi basi na ajiandae, makazi yake ni motoni".

Imepokelewa kutoka kwa Mikdad Bin Maadi Karbi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kwa hakika imefikia wakati ambao mtu atafikiwa na hadithi yangu akiwa amekaa kwenye tandiko lake na akisema: Hakika kitakachotuhukumu kati yetu ni kitabu cha Mwenyezi Mungu hivyo tukikuta halali ndani yake tutaihalalisha na tukikuta ndani yake kuna haramu tutaiharamisha, na kwa hakika chochote alichokiharamisha Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na amani ziwe juu yake ni kama alichokiharamisha Mwenyezi Mungu".

Kutoka kwa Aisha na Abdillah bin Abbasi -Radhi za Allah ziwe juu yao wamesema: Yalipomfika Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mauti akawa anaweka nguo yake juu ya uso wake, anapozidiwa kupumua anaifunua kutoka usoni kwake, na anasema naye akiwa katika hali hiyo: "Laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mayahudi na Maswara, waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa ni Misikiti" Akitahadharisha waliyoyafanya.

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Ewe Mwenyezi Mungu, usilifanye kaburi langu kuwa ni sanamu, Allah amewalaani watu walioyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa misikiti".

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, na wala msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, na nitakieni rehema, kwani dua zenu hunifikia mahala popote muwapo".

Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mama Salama alimsimulia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kisa cha kanisa aliloliona katika ardhi ya Ethiopia, likiitwa kanisa la Mtakatifu Maria, akasimulia aliyoyaona ndani yake miongoni mwa picha, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Watu hao anapokufa kwao mja mwema, au mwanaume mwema, wanajenga juu ya kaburi lake mahala pakuabudia, na wanachora ndani yake picha hizo, hao ndio viumbe waovu zaidi mbele ya Allah