- Himizo la kufikisha sheria ya Allah, nakuwa mtu anajukumu la kuyafikisha aliyoyahifadhi na kuyaelewa hata kama ni kidogo.
- Ulazima wa kutafuta elimu ya kisheria, ili mtu awe na uwezo wa kumuabudu Allah na kuifikisha sheria yake kwa sura sahihi.
- Uwajibu wa kuhakiki usahihi wa kila hadithi kabla ya kuifikisha au kuisambaza kwa kutahadhari kutoingia katika ahadi hii ya adhabu kali.
- Himizo la ukweli katika maneno, na kuchukua tahadhari katika mazungumzo, ili mtu asiingie katika uongo, na hasa hasa katika sheria ya Allah -Aliyetakasika na kutukuka-.