- Tunapaswa kuzingatia kile ambacho ni muhimu zaidi na kinachohitajika, na kuacha kile kisichohitajika mara moja, na tusijishughulishe na kuuliza juu ya kile ambacho hakijatokea.
- Ni haramu kuuliza maswali ambayo yanaweza kutatiza baadhi ya mambo, na kufungua mlango wa shaka ambayo husababisha kuhitilafiana kwingi.
- Amri ya kuacha makatazo yote; Kwa sababu hakuna ugumu katika kuyaacha, na ndiyo maana katazo lilikuja kwa ujumla.
- Amri ya kufanya kile kilichoamrishwa ni kwa kadiri ya uwezo; Kwa sababu mtu inaweza kuwa vigumu kwake kuitekeleza au akashindwa kuifanya; ndio maana amri ilikuja kuwa ifanyike kwa kadiri ya uwezo.
- Katazo la kuuliza maswali mengi Wanachuoni wamegawanya kuuliza katika sehemu mbili: Moja wapo: Ni maswali yanayokuwa katika mfumo wa kujifunza yale anayoyahitajia mtu kuhusiana na mambo ya dini, hili limeamrishwa, na miongoni mwa aina hii ni maswali ya Maswahaba, na aina ya pili: Ni maswali yanayokuwa katika sura ya kiburi na kujikalifisha, na hii ndiyo iliyoharamishwa.
- Tahadhari kwa Umma huu dhidi ya kumpinga Nabii wake, kama ilivyotokea katika Umma zilizokuwa kabla yake.
- Maswali mengi juu ya mambo yasiyohitajika na kutofautiana na mitume ni sababu ya maangamizo, na hasa katika mambo ambayo hayawezi kufikiwa, kama vile: Masuala ya ghaibu ambayo Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayeyajua, na hali za Siku ya Kiyama.
- Katazo la kuuliza maswali katika mambo magumu, amesema Auzaai: Hakika Mwenyezi Mungu akitaka kumnyima mja wake baraka ya elimu, anaweka upotovu katika ulimi wake, na niliwaona watu wa namna hivyo kuwa ni watu wasio na elimu, na amesema bin Wahabi: Nilimsikia Maliki akisema: Mijadala tasa katika elimu hunaondoa nuru ya elimu katika moyo wa mtu.