- Kuvuka mpaka wa kisheria katika makaburi ya Manabii na watu wema hufanya yaabudiwe kinyume na Mwenyezi Mungu, ni lazima kuchukua tahadhari na njia zinazopelekea katika ushirikina.
- Haifai kwenda makaburini kwa lengo la kuyatukuza na kufanya ibada hapo, vyovyote vile utakavyokuwa ukaribu wa mwenye kaburi na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Uharamu wa kujenga misikiti juu ya makaburi.
- Uharamu wa kuswali makaburini hata kama hujajengwa msikiti hapo, isipokuwa swala ya jeneza ambalo halijaswaliwa (wanaweza kuswalia kwa dharura hiyo)