- Tahadhari ya kuvuka mpaka wa kisheria katika kuzikuza sifa; kwani hilo hupelekea katika ushirikina.
- Aliyoyatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- tayari yamekwisha tokea katika umma huu, kundi likachupa mipaka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kundi kwa watu wa nyumba yake, na kundi kwa mawalii wake (wacha Mungu), wakatumbukia katika ushirikina.
- Amejisifu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu; ili aweke wazi kuwa yeye ni mja anaelelewa na Mwenyezi Mungu haifai kuelekezewa chochote katika mambo mahususi ya kiuungu.
- Amejisifu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu; ili aweke wazi kuwa yeye katumwa kutoka kwa Allah hivyo, ni wajibu kumsadikisha na kumfuata.