- Kukatazwa kuyafanya makaburi ya Manabii na watu wema kuwa Misikiti inayoswaliwa kwaajili ya Mwenyezi Mungu, kwasababu hilo ni njia inayopelekea katika ushirikina.
- Kipaumbele kikubwa cha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuitilia umuhimu tauhidi na hofu yake juu ya kutukuzwa makaburi; kwa sababu hilo linapelekea katika ushirikina.
- Inafaa kuwalaani Mahayudi na Manaswara na atakayefanya mfano wa vitendo vyao ikiwemo kuyajengea makaburi na kuyafanya kuwa mahali pa ibada.
- Kujengea makaburi ni katika taratibu za Mayahudi na Manaswara, na katika hadithi hii kuna katazo la kujifananisha nao.
- Miongoni mwa kuyafanya makaburi kuwa misikiti ni kuswali hapo au kuswali kwa kuyaelekea, hata kama hapajajengwa msikiti.