Kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mwenyezi Mungu alipoumba Pepo na Moto alimtuma...
Alitoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu alipoumba Pepo na Moto, alimwambia Jibril -Amani iwe juu yake- nenda mpaka P...
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Moto wenu wa Dunia ni sawa na sehemu t...
Anatoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Moto wa Duniani ni sehemu moja tu kutoka katika Moto wa Jahannam, Hivyo basi moto wa Akhera u...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Ataikamata Mwen...
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu Mtukufu ataikamata Ardhi na kuikusanya, na ataikunja Mbingu kwa mkon...
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alingia kwangu Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikiwa nimeweka...
Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliingia nyumbani kwake kwa Aisha radhi za Allah ziwe juu yake akamkuta akiwa kafunika ghala dogo ambalo huhifadhi...
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Namuapa yule ambaye nafsi ya...
Anaapa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya ukaribu wa kuteremka Issa mwana wa Mariam amani iwe juu yake ili ahukumu baina ya watu kwa uadilif...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mwenyezi Mungu alipoumba Pepo na Moto alimtuma Malaika Jibril -Amani iwe juu yake- aende peponi Akamwambia: Iangalie hiyo pepo na yale niliyo waandalia humo watu wa peponi, basi Jibrili akaiangalia Pepo kisha akarudi, akasema: Naapa kwa utukufu Wako ewe Mwenyezi Mungu hatozisikia mtu yeyote habari za pepo kisha asiingie humo, kisha akamuamrisha kuizungushia Pepo hiyo mambo yenye kuchukiza, kisha akamwambia nenda tena ukaiangalie na uangalie yale niyowaandalia watu wake humo peponi. Basi akaiangalia ghafla akaiona imezungushwa vyenye kuchukiza, akasema: Naapa kwa utukufu Wako kwa hakika ninahofia kuwa hatoingia mtu yeyote. Akasema kumwambia Jibrili nenda na uuangalie Moto na yale niliyo waandalia humo watu wa Motoni. Basi akauangalia Moto na akauona Moto ulivyopambwa, basi akarudi na akasema: Naapa kwa utukufu Wako hatoingia yeyote humo, basi akaamrisha ukazungushwa mambo yenye kutamanisha, basi akamwambia: Rudi na uuangalie tena. Basi akauangalia akaukuta umepambwa na kuzungushwa yenye kutamanisha, basi akarudi na akasema: Naapa kwa utukufu wako kwa hakika nahofia yakuwa hatosalimika mtu yeyote isipokuwa ataingia Motoni."

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Moto wenu wa Dunia ni sawa na sehemu tu ya sabini itokanayo na moto wa Jahannam" Kukasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ikiwa ni hivyo basi moto wa Duniani unatosha kuadhibu, akasema: "Umeongezewa ukali zaidi yake kwa mara sitini na tisa, na mara zote hizo sitini na tisa kila mara moja ni sawa na ukali wa moto wa duniani."

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Ataikamata Mwenyezi Mungu ardhi, na ataikunja mbingu kwa mkono wake wa kulia kisha atasema: Mimi ndiye Mfalme; wako wapi wafalme wa ardhi?"

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alingia kwangu Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikiwa nimeweka pazia lenye picha kwa kusahau, alipoliona akalichana na akaghadhibika mpaka uso wake ukabadilika rangi, na akasema: "Ewe Aisha, Watu wenye adhabu kali zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama, ni wale wenye kutengeneza mfano wa vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu" Aisha anasema: "Tukalichana vipande vipande vingine tukavifanya kuwa mto au mito miwili ya kulalia".

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hivi karibuni atakuteremkieni Issa mwana wa Mariam atakuwa hakimu na muadilifu, atavunja misalaba, na ataua nguruwe, na ataweka kodi (Jizia), na mali itabugujika (itakuwa nyingi) mpaka itafikia mahali hakuna yeyote atakayeikubali".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimwambia baba yake mdogo: "Sema: Laa ilaaha illa llahu, nitakutolea ushuhuda wa kusilimu kwa maneno hayo siku ya Kiyama" Akasema: Ningetamka kama si kuogopea matusi ya Makuraishi wanasema kulichompelekea kusema maneno hayo ni kuogopa kifo, kama si hivyo ningeingiza furaha moyoni mwako, basi Mwenyezi Mungu akateremsha: "Hakika wewe huwezi kumuongoza umtakaye lakini Mwenyezi Mungu humuongoza amtakaye" (suratul Qaswas: 56)

Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Amrou -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Birika langu ukubwa wake ni sawa na mwendo wa mwezi mzima, maji yake ni meupe kuliko maziwa, na harufu yake ni nzuri kuliko ya Miski, Vikombe vyake ni kama idadi ya nyota za mbinguni, yeyote atakaye kunywa kwenye birika hilo hatopatwa na kiu milele"

Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mauti yataletwa yakiwa kama dume la Kondoo mwenye rangi mchanganyiko ya weusi na weupe,kisha muitaji ataita; Enyi watu wa peponi, basi watainua vichwa vyao na kuangalia, basi mwenye kuita atasema: Je mnamjua huyu? Nao watajibu: Ndiyo hayo ni Mauti, na wote kwa hakika wameyaona, kisha mwenye kuita atawaita: Enyi watu wa Motoni, basi watainua shingo zao na kuangalia, basi atawaambia na je mnamjua huyu basi watamjibu ndiyo haya ni Mauti, na wote kwa kakika wameyaona, hivyo basi yatachinjwa kisha atasema: Enyi watu wa Peponi,kaeni humo milele na hakuna kufa, na nyie watu wa motoni kaeni humo milele na hakuna kufa, kisha akasoma: "Na uwaonye siku ya majuto wakati hukumu ya kuingia peponi na motoni itakapotolewa Nao wapo kwenye kughafilika na wala hawaamini" (Surat Maryam:39)

imepokewa Kutoka kwa Omari bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake-: Hakika yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Lau kama nyinyi mngelimtegemea Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea, basi angekuruzukuni kama anavyomruzuku ndege, anatoka asubuhi akiwa na njaa anarudi mchana akiwa kashiba".

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Neema mbili wamepoteza thamani yake watu wengi: Afya na wakati".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Amsalimie aliyepanda anayetembea, na anayetembea aliyekaa, na wachache kwa wengi"

Imepokewa kutoka kwa Abuu Dharri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-katika yale aliyoyapokea kutoka kwa Mola wake Mtukufu hakika Yeye amesema: "Enyi waja wangu hakika Mimi nimeharamisha dhulma juu ya Nafsi yangu na nikaifanya kuwa ni haramu baina yenu, basi msidhulumiane, enyi waja wangu nyote ni wapotevu isipokuwa yule niliye muongoza, basi niombeni uongofu nami nitakuongozeni, enyi waja wangu nyote ni wenye njaa isipokuwa yule niliye mlisha, basi niombeni chakula nami nitakulisheni, enyi waja wangu nyote mpo uchi isipokuwa yule niliye mvisha, basi niombeni kuvaa nami nitakuvisheni, enyi waja wangu hakika nyinyi mnakosea usiku na mchana na mimi ninasamehe madhambi yote, basi niombeni msamaha nami nitakusameheni, enyi waja wangu hamtafikia kufanya madhara ili mnidhuru wala hamtafanya mambo yenye manufaa ili mninufaishe, enyi waja wangu laiti wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu binadamu na majini wakijikusanya wote wakawa na ucha Mungu wa mtu mmoja hilo lisinge niongezea chochote katika Ufalme wangu chochote, enyi waja wangu laiti wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu binadamu na majini wakijikusanya wote wakafanya uovu wa mtu mmoja hilo lisinge punguza chochote katika Ufalme wangu, enyi waja wangu laiti wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu binadamu na majini wangejikusanya katika uwanja mmoja wakaniomba nikampa kila mtu alicho kiomba hilo lisinge punguza chochote katika Ufalame wangu isipokuwa ni kama sindano inavyo punguza maji pindi inapo ingizwa baharini, enyi waja wangu si vinginevyo bali hakika matendo yenu yote nina wahifadhieni kisha nitawapa malipo yenu, mwenye kupata kheri amshukuru Mwenyezi Mungu, na atakayepata kinyume na hayo basi asimlaumu yeyote isipokuwa nafsi yake."