- Kumfananisha mtu mzima na mfanya biashara, na afya na muda kavifananisha na mtaji; atakayeutumia vizuri mtaji wake atapata faida, na atakayeupoteza basi atapata hasara na kujuta.
- Amesema bin Khaazin: Neema ni kila anachoneemeka nacho mtu na anapata ladha kwacho, na udanganyifu, ni mtu kununua kitu kwa thamani kubwa, au kukiuza kwa thamani isiyolingana na kilichouzwa; atakayekuwa na afya katika mwili wake na akawa na wakati na hana la kumshughulisha, na akawa hakwenda mbio kuitumikia Akhera yake huyu ni sawa na aliyefanya biashara yenye udanganyifu.
- Kuwa na pupa ya kufaidika na afya na wakati kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na Kutukuka, na kufanya kheri kabla ya kutoweka kwake.
- Kushukuru neema za Mwenyezi Mungu kunakuwa kwa kuzitumia katika kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Amesema Kadhi Abubakari bin Al-Arabi: Kumepatikana tofauti kuwa ni ipi neema ya kwanza kwa mja, kukasemwa: Ni imani, na kukasemwa: Ni uhai, na kukasemwa: Ni afya, na ya kwanza ndio bora kwa sababu ndio neema ya kiujumla, na ama uhai na afya hizo ni neema za kidunia, na wala haziwezi kuwa neema halisia isipokuwa zitakapoambatana na imani, na hapo ndipo wanapohadaika watu wetu, yaani inapotea faida yao au inapungua, atakayeiendekeza nafsi yake yenye kuamrisha maovu, na yenye kudumu katika starehe, akaacha kuhifadhi mipaka ya Mwenyezi Mungu, na kudumu na ibada, basi huyu atakuwa kahadaika, na vile vile atakapokuwa hana la kumshughulisha, kwa sababu aliyeshughulishwa anaweza kuwa na udhuru tofauti na mwenye nafasi; basi huyu hana udhuru na hoja itasimama juu yake.