- Kuamini kuwa Pepo na Moto kwa sasa vyote hivyo vipo.
- Ulazima wa kuamini mambo ya ghaibu (yasiyo onekana), na kuamini kila kilichokuja kutoka kwa, Mwenyezi Mungu na Mtume wake -Rehema na amani ziwe juu yake-.
- Umuhimu wa kusubiri kwenye mambo yenye kuudhi kwa sababu hiyo ni njia ya kumfikisha mtu peponi.
- Umuhimu wa kujiepusha na mambo yaliyoharamishwa; kwa sababu hiyo ni njia ya kumfikisha mtu Motoni.
- Pepo imezungushwa yenye kuchukiza, na Moto umezungushwa yenye kutamanisha, nayo hupelekea kuingia kwenye majaribu katika maisha haya ya Duniani.
- Njia ya kwenda Peponi ni ngumu na ina tabu nyingi, na inahitajia subira kuvumilia mateso pamoja na kuwa na imani, na njia ya kwenda Motoni imejaa vyenye kuvutia na kutamanisha hapa duniani.