Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Amesema: "Mtu huwa katika mwenendo wa rafiki yake wa...
Alibainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mtu hufanana na rafiki na jamaa yake wa dhati katika nyenendo na tabia zake, na urafiki huathiri...
Kutoka kwa Mughira bin Shuuba -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Halitoacha kuendelea kudhihiri...
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwa hawatoacha watu katika Umma wake kuendelea kuwepo, na kuwashinda wanaopingana nao, na hilo litaen...
Imepokelewa kutoka kwa Tamim Ad-Dari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake...
Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie, amesema kuwa dini hii itaenea sehemu zote za ardhi, hivyo dini hii itafika sehemu yoyote ile ufikap...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Ulianza Uislamu ukiwa ni m...
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Uislamu ulianza ukiwa kwa mtu mmoja mmoja na uchache wa watu wake, na utarejea ukiwa mgeni kwa...
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -sala na amani ziwe juu yake- amesema: "Namuapa yule ambaye nafsi ya...
Anaapa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna atayemsikia katika umma huu, Myahudi au Mkristo au mwingine yeyote utakayemfikia ujumbe wa Mt...

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Amesema: "Mtu huwa katika mwenendo wa rafiki yake wa karibu, basi na aangalie mmoja wenu ni nani anayemfanya kuwa rafiki yake"

Kutoka kwa Mughira bin Shuuba -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Halitoacha kuendelea kudhihiri kundi katika Umma wangu, mpaka iwajie amri ya Mwenyezi Mungu nao wakiwa katika kudhihiri huko".

Imepokelewa kutoka kwa Tamim Ad-Dari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Litafikia jambo hili ulipofika usiku na mchana, na wala hatoacha Mwenyezi Mungu nyumba ya mjini wala ya kijijini isipokuwa ataiingiza Mwenyezi Mungu dini hii, kwa utukufu wa yeyote au kwa udhalili wa yeyote, ni utukufu anaoutukuza Mwenyezi Mungu uislamu, na ni udhalili anaoudhalilisha Mwenyezi Mungu ukafiri" na alikuwa Tamimu Dari akisema, nililijua hilo kwa watu wa familia yangu, kwa hakika alipata aliyesilimu miongoni mwao kheri na heshima na utukufu, na aliyekuwa kafiri alipata udhalili na unyonge na ulipaji kodi.

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Ulianza Uislamu ukiwa ni mgeni na utarudi kuwa mgeni kama ulivyo anza, basi shangwe kwa wale wanaoonekana kuwa ni wageni".

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -sala na amani ziwe juu yake- amesema: "Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hatonisikia yeyote katika umma huu, Myahudi wala Mkristo, kisha akafa haliyakuwa hajayaamini yale niliyotumwa kwayo, isipokuwa atakuwa ni katika watu wa motoni".

Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake asubuhi ya tukio la Akaba huku akiwa juu ya Ngamia wake: "Niokotee kijiwe" Nikamuokotea vijiwe saba, navyo ni vijiwe vya kurusha wakati wa kuwinda, akawa akivipuliza katika kiganja chake huku akisema: "Mfano wa vijiwe hivi basi rusheni" Kisha akasema: "Enyi watu, tahadharini sana na kuchupa mipaka katika dini, kwani kilichowaangamiza waliokuwa kabla yenu ni kuchupa mpaka katika dini".

Kutoka kwa Abdallah Ibn Masoud amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Wameangamia wenye kufanya uzito katika mambo" Alisema hivyo mara tatu.

Kutoka kwa Adiy bin Hatim kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mayahudi wameghadhibikiwa, na Wakristo ni wapotofu".

Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Amrou Bin Aaswi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Aliandika Mwenyezi Mungu makadirio ya viumbe kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini, akasema: Na Arshi yake ilikuwa juu ya maji."

Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Ametuhadithia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- naye ni mkweli mwenye kukubaliwa: "Kwa hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake kwenye tumbo la mama yake mchana arobaini na nyusiku arobaini kisha anakuwa tone la manii kwa muda kama huo kisha anakuwa pande la damu kwa mfano wa siku hizo, kisha hutumwa Malaika na huamrishwa kufanya mambo manne; Hivyo basi ataandika riziki yake, na muda wa kufa kwake na matendo yake na ataandika kuwa ni muovu au ni mwema, kisha atampulizia roho, na kwa hakika mmoja wenu anaweza kufanya matendo ya watu wa Peponi kiasi ya kuwa haitobakia kati yake na kuingia Peponi isipokuwa usawa wa urefu wa mkono, basi kikamtangulia kitabu -Kadari- na akafanya matendo ya watu wa motoni na akaingia motoni, na kwa hakika mmoja wenu anaweza akafanya matendo miongoni mwa matendo ya watu wa motoni mpaka ikabakia kati yake na kuingia motoni kiasi cha usawa wa mkono kisha kikamtangulia kitabu -Kadari- akafanya mataendo ya watu wa peponi na akaingia peponi."

Imepokelewa Kutoka kwa Ibn Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Pepo iko karibu mno kwa mmoja wenu kuliko umbali wa kanyagio la kiatu na kisigino chake, na moto pia hivyo hivyo".

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Moto umezingirwa na yenyekutamanisha, na Pepo imezingirwa na yenyekuchukiza".