- Uharamu wa misimamo mikali katika mambo yote, na himizo la kuepuka hilo katika kila kitu; hasa hasa katika ibada na kuwatukuza watu wema.
- Kutafuta ukamilifu katika ibada na mengine mazuri; na kunakuwa kwa kufuata sheria.
- Inapendeza kulitilia mkazo jambo muhimu, kwa sababu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikariri sentensi hii mara tatu.
- Upole wa uislamu na wepesi wake.