- Kuenea kwa ujumbe wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa ulimwengu mzima, na ulazima wa kumfuata kwake, na kufutwa kwa sheria zote kupitia sheria yake.
- Atakayempinga Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hayatomfaa kitu madai yake ya kudai kumwamini Nabii mwingine katika Manabii -Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yao wote-.
- Ambaye hakumsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na haukumfikia ujumbe wa Uislamu huyu atapewa udhuru, na hukumu yake huko Akhera itakuwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Yanathibitika manufaa kwa Uislamu kwa mtu hata kama atasilimu muda mchache kabla ya kifo, hata kama atakuwa katika maradhi mabaya, madama tu roho haijafika kooni.
- Kuiona kuwa ni sahihi dini ya makafiri -wakiwemo Mayahudi na Wakristo- ni ukafiri.
- Amemtaja Myahudi na Mkristo katika hadithi kama tahadhari kwa wenye kuwaona kuwa wako sawa; na hii ni kwakuwa Mayahudi na Wakristo wana kitabu, na ikiwa ndio hivyo, basi kwa wengine wasiokuwa na kitabu ndio wanastahiki zaidi kuingia motoni, wote hao wanalazimika kuingia katika dini yake na kumtii yeye Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.