Na kutoka kwa Jaabir Bin Abdillah -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu...
Alitahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu dhulma, ikiwemo: Kuwadhulumu watu na kujidhulumu mwenyewe na kufanya dhulma katika haki ya...
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Musa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu humpa mud...
Anatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutokuendelea kubaki katika dhulma kwa kufanya maasi na ushirikina na kuwadhulumu watu haki zao,...
Imepokewa Kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake- Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika yale anayoyapok...
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu amepanga mema na maovu, kisha akawabainishia Malaika wawili ni namna gani wata...
Imepokelewa hadithi kutoka kwa bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, amesema: Alisema mtu mmoja: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hivi sisi...
Anatuwekea wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ubora wa kuingia katika Uislamu, Na kuwa mwenye kusilimu na uislamu wake ukawa mzuri na akawa mt...
Imepokewa kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Yakwamba watu miongoni mwa washirikina walikuwa wameuwa watu, na wakak...
Walikuja watu miongoni mwa washirikina kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na walikuwa wamekwisha fanya mauaji mengi na zinaa nyingi, wakasema k...
Na kutoka kwa Jaabir Bin Abdillah -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- "Ogopeni dhulma, kwa hakika dhulma ni giza siku ya kiyama. Na ogopeni tamaa, kwa hakika tamaa iliwaangamiza walio kuwepo kabla yenu. Iliwapelekea kumwaga damu zao, na kuhalalisha yaliyo haramu kwao".
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Musa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu humpa muda dhalimu, mpaka akija kumuadhibu hambakishi" Anasema: Kisha akasoma: "Na hivyo ndivyo kuadhibu kwa Mola wako Mlezi anapoikamata miji inapokuwa imedhulumu. Hakika mkamato wake ni mchungu na mkali" [Hud:102]
Imepokewa Kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake- Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika yale anayoyapokea kutoka kwa Mola wake Mtukufu amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu amepanga mema na mabaya, kisha akalibainisha hilo, atakayekusudia kufanya jema akawa hakulifanya Mwenyezi Mungu humuandikia jema moja kamili, ikiwa atapania na akalifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake mema kumi mpaka ziada ya mia saba, mpaka kufikia nyongeza ya juu zaidi, na atakayekusudia jambo baya na akawa hakulifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake jema moja kamili, ikiwa atapania na akalifanya Mwenyezi Mungu humuandikia kwake dhambi moja."
Imepokelewa hadithi kutoka kwa bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, amesema: Alisema mtu mmoja: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hivi sisi tutaadhibiwa kwa tuliyoyafanya katika zama za ujinga kabla yakuwa waislamu?Akasema "Yeyote atakayefanya wema katika Uislamu basi hatoadhibiwa kwa yale aliyoyatenda katika zama za ujinga, na yeyote atakaye tenda maovu akiwa katika Uislamu ataadhibiwa kwa makosa yake ya mwanzo na ya mwisho".
Imepokewa kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Yakwamba watu miongoni mwa washirikina walikuwa wameuwa watu, na wakakithirisha mauaji, na wakazini na wakikithirisha zinaa, wakamjia Muhammadi -Rehema na amani ziwe juu yake- wakasema: Hakika haya unayoyasema na kuwalingania watu ni mambo mazuri, ikiwa utatwambia juu ya haya tuliyoyafanya kama yana kafara, ikateremka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na wale ambao hawamuombi pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwingine na wala hawauwi nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa haki na wala hawazini" [Al-Furqan: 68], na ikateremka: "Sema: Enyi waja wangu waliojidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu..." [Az-Zumar: 53].
Imepokelewa kutoka kwa Hakiim Bin Hizaam -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni upi mtazamo wako katika mambo ambayo nilikuwa nikifanya ibada kupitia mambo hayo kabla ya kuwa muislamu, miongoni mwa sadaka, au kumwacha huru mtumwa, au kuunganisha udugu, je katika mambo hayo kuna malipo? Basi akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: " Umekwisha pokea malipo yako kutokana na mema uliyoyatanguliza".
Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Kwa hakika Mwenyezi Mungu hamdhulumu muumini kwa jema alilofanya, huandikiwa thawabu za wema wake hapa Duniani na hulipwa thawabu hizo huko Akhera Ama kafiri hulishwa kwa mema aliyoyafanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hapa duniani, mpaka akifika Akhera anakuwa hana jema lolote ambalo atalipwa nalo."
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: “Amesema Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka: “Ewe mwanadam, maadamu unaniomba na kunitumainia, nitakusamehe uliyo nayo wala sitojali Ewe mwanadam lau madhambi yako yangefika mawinguni kisha ukaniomba msamaha ningekusamehe wala sijali Ewe mwanadam, lau ungenijia na thamani ya dhambi za dunia, kisha ukakutana nami bila kunishirikisha na chochote, ningekuletea msamaha ujazo sawa na ardhi".
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, katika yale anayoyasimulia kutoka kwa Mola wake Mtukufu, amesema: "Mja alifanya dhambi akasema: Ee Mola wangu nisamehe dhambi yangu, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, na humsitiri kwa ndambi hiyo au humuadhibu kwa kutenda dhambi, kisha akarudi tena akatenda dhambi, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe dhambi yangu, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, na ana adhibu kwa kutenda dhambi, fanya utakavyo nimekusamehe".
Kutoka kwa Ally amesema: Hakika mimi nilikuwa ni mtu kila nikisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hadithi Mwenyezi Mungu ananinufaisha kwa hadithi hiyo kwa kiasi alichotaka kuninufaisha, na akinihadithia yeyote katika Masahaba zake ninamuapisha, akiniapia ninamuamini, na siku moja alinihadithia Abubakari, na Abubakari akasema ukweli, akasema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakuna mtu yeyote atakayetenda dhambi, kisha akasimama akajitwaharisha, kisha akaswali, kisha akamuomba Allah msamaha, isipokuwa Mwenyezi Mungu humsamehe", Kisha akasoma aya hii: "Na wale ambao wakifanya machafu au wakizidhulumu nafsi zao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakaomba msamaha kutokana na madhambi yao" [Al-Imran: 135].
Na kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyoosha mkono wake wakati wa usiku ili amsamehe mkosefu wa mchana, na ananyoosha mkono wake wakati wa mchana ili amsamehe mkosaji wa usiku, mpaka jua litakapochomoza kutoka magharibi yake."
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Anateremka Mola wetu Mlezi -Aliyetakasika na kutukuka- katika mbingu ya dunia pindi inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku, husema: "Ni nani anayeniomba nimjibu? Ni nani anayenitaka shida yake nimpe? Ni nani anayeniomba msamaha nimsamehe?".