- Ubora wa Uislamu na utukufu wake nakuwa Uislamu unabomoa madhambi yaliyokuwa kabla yake.
- Upana wa rehema ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake na msamaha wake na kufuta kwake madhambi.
- Uharamu wa ushirikina, na uharamu wa kuua nafsi bila hatia, na uharamu wa zinaa, na ahadi ya adhabu kwa atakayeyasogelea ama kujiingiza katika madhambi haya.
- Toba ya kweli iliyoambatana na utakasifu (Ikhlaswi) na matendo mema, hufuta madhambi yote makubwa likiwemo la kumkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Uharamu wa kukata tamaa na kunyongeka katika rehema za Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.