- Kukubaliwa toba kunaendelea maadamu mlango wake uko wazi, na mlango wake utafungwa wakati jua linapochomoza kutoka magharibi, na kwamba mtu atubu kabla ya msukosuko wa kifo, ambao ni roho kufika kooni.
- Kutokata tamaa kwa sababu ya dhambi, kwani msamaha na rehema za Mwenyezi Mungu ni mpana, na mlango wa toba uko wazi.
- Masharti ya kutubia: La kwanza: kuacha dhambi, la pili: kujuta kwa kuitenda, na la tatu: kuazimia kutorejea tena, ikiwa ni katika haki za Mwenyezi Mungu, na ikiwa inahusiana na haki za waja, basi kwa ajili ya kupokelewa toba inatakiwa kuwa haki hiyo apewe mmiliki wake au mwenye haki amsamehe.