- Upana wa huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake na kuwa mwanadamu vyovyote vile atakavyotenda dhambi, vyovyote vile atakavyofanya, atakapotubia kwake na akarejea basi Mwenyezi Mungu humsamehe.
- Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu hutumai kupata msamaha wa Mola wake Mlezi, na huogopa adhabu yake, hivyo huenda mbio kutubia na wala haendelei kubaki katika maasi.
- Sharti za toba sahihi: Ni kujiondoa katika dhambi, na kulijutia, na kutia nia ya kutolirudia dhambi, na toba ikiwa ni katika mali za watu au heshima zao au nafsi, hapo huongezeka sharti la nne, nalo: Ni kujivua kutoka kwa mwenye haki yake, au kumpa haki yake.
- Umuhimu wa elimu ya kumjuwa Mwenyezi Mungu elimu ambayo humfanya mja kujua mambo ya dini yake, akatubia kila anapokosea, hakati tamaa wala hafanyi jeuri kwa kuendelea kubaki katika dhambi.