Imepokewa Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: Nuuman akash...
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kanuni kuu katika mambo, nakuwa zinagawanyika sehemu tatu katika sheria: Halali ya wazi, na haramu...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiwatu...
Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwatukana Maswahabah hasa wa mwanzo katika Muhajirina na Ansari; na akaeleza kuwa lau mmoja miongoni mw...
Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema: Siku moja nilikuwa nyuma ya Mtume -Rehema na amani ziwe j...
Anaeleza bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yake- kuwa yeye alipokuwa kijana mdogo alikuwa kapanda pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, ak...
Kutoka kwa Sufiani bin Abdillah Al-Thaqafi Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Nieleze ndani ya Uislamu kau...
Swahaba Sufiani bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake alimuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amfundishe kauli iliyokusanya maana nzima ya...
kutoka kwa Nu'man Bin Bashiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake -: "Mfano wa waum...
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa inatakiwa kuwa hali ya waislamu baadhi yao kwa baadhi katika kupendeleana kheri na kuhurumiana...
Imepokewa Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: Nuuman akashusha vidole vyake masikioni mwake-" "Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi na kati ya halali na haramu kuna mambo yenye kutatiza, hawayajui mambo hayo wengi miongoni mwa watu, atakaye yaepuka mambo yenye kutatiza, basi atakuwa kaihifadhi dini yake na heshima yake, na atakayeingia katika mambo yenye kutatiza atakuwa kaingia katika haramu, ni kama mfano wa mchunga mifugo mwenye kuchungia kando kando ya mipaka wanahofiwa (mifugo wake) kuingia humo, tambueni na hakika kila Mfalme ana mipaka yake, na tambueni kuwa mipaka ya Mwenyezi Mungu ni makatazo yake, na tambueni kuwa katika mwili kuna kipande cha nyama, kikitengemaa mwili mzima unatengemaa, na kikiharibika, mwili mzima unaharibika, tambueni kipande hicho ni moyo."
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiwatukane Maswahaba wangu, kwa sababu, lau kama yeyote kati yenu atatoa dhahabu sawa na (mlima) Uhud (katika njia ya Mwenyezi Mungu), basi haiwezi kuwa sawa na theluthi mbili ya kilo ya mmoja wao wala nusu yake."
Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema: Siku moja nilikuwa nyuma ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: "Ewe kijana, hakika mimi ninakufundisha maneno, muhifadhi Mwenyezi Mungu naye atakuhifadhi, muhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta uendako, utakapoomba basi muombe Mwenyezi Mungu, na utakapotaka msaada basi taka msaada kwa Mwenyezi Mungu, na tambua kuwa umma mzima lau wangekusanyika ili wakunufaishe kwa chochote, basi wasingelikunufaisha isipokuwa kwa kitu alicho kuandikia Mwenyezi Mungu kuwa chako, na lau kama wangelikusanyika ili wakudhuru kwa chochote, basi wasingeweza kukudhuru isipokuwa kwa kitu alichokiandika Mwenyezi Mungu dhidi yako, kalamu zimenyanyuliwa na kurasa zimekauka".
Kutoka kwa Sufiani bin Abdillah Al-Thaqafi Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Nieleze ndani ya Uislamu kauli ambayo sitomuuliza yeyote zaidi yako, akasema: "Sema: Nimemuamini Mwenyezi Mungu, kisha kuwa na msimamo".
kutoka kwa Nu'man Bin Bashiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake -: "Mfano wa waumini katika kupendana kwao na kuhurumiana kwao na kufanyiana kwao upole, ni kama mfano wa kiwiliwili, kinapopata tabu kiungo kimoja vinaitana kwa ajili ya hicho kimoja viungo vyote kwa kukesha na maumivu".
Imepokelewa kutoka kwa Othman bi Affan -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu wake, hutoka makosa yake ndani ya mwili wake mpaka yakatiririka kutoka chini ya kucha zake".
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika sisi tunasafiri Baharini, na tunabeba maji kidogo sana, tukiyatumia kutawadha tunakosa maji ya kunywa, je, tunaweza kutawadha kwa maji ya Bahari? Akasema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Ni safi Maji yake na ni halali mizoga yake".
Kutoka kwa Abdallah bin Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao amesema: Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu maji, na vile vinavyoyaendea kama wanyama wa kawaida na wanyama pori, akasema rehema na amani ziwe juu yake: "Maji yatakapokuwa ni kulataini (Mapipa mawili) basi hayashiki uchafu".
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ayub Al-Answari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: “Mnapoingia chooni, msielekee Kibla, wala msikipe mgongo, bali elekeeni Mashariki au Magharibi.” Abuu Ayub akasema: Basi tukaenda Sham tukakuta vyoo vimejengwa kuelekea Kibla, tukawa tunageuka, na tunaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Kutoka kwa Abuu Katada -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Asishike mmoja wenu utupu wake kwa mkono wake wa kulia akiwa anakidhi haja ndogo, na asijifute haja ndogo au kubwa kwa mkono wake wa kulia na asipumulie ndani ya chombo anachonywea."
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapoamka mmoja wenu kutoka usingizini mwake basi na apenge kwa maji mara tatu, kwani Shetani hulala ndani ya tundu zake za pua".
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiosha, au akioga, kwa kibaba kimoja mpaka vibaba vitano, na anatawadha kwa kibaba kimoja.