- Msingi wa Dini ni kumuamini Mwenyezi Mungu kwa Ulezi wake na uungu wake na majina yake na sifa zake.
- Umuhimu wa kuwa na msimamo baada ya kuamini, na kudumu na ibada na kuthubutu juu ya hilo.
- Imani ni sharti la kukubaliwa matendo.
- Kumuamini Mwenyezi Mungu kunakusanya yote yanayopaswa kuitakidi miongoni mwa itikadi za imani na misingi yake, na yanayofuata hilo miongoni mwa amali za moyo, na kutii na kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa siri na kwa wazi.
- Msimamo ni kubaki katika njia, kwa kutekeleza wajibu na kuacha makatazo.