Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Ilikuwa Dua aiombayo zaidi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:ni "Ewe...
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikithirisha dua kwa dua fupi zenye kukusanya mambo mengi, na miongoni mwake: "Ewe Mwenyezi Mungu! Tupe h...
Kutoka kwa Abuu Dardaa -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Je,...
Maswahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: . Hivi je mnata nikuelezeni na nikufundisheni amali bora zaidi kuliko zote katika amali...
Kutoka kwa Muadhi bin Jabali -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, nikajikuta...
Amesema Muadhi radhi za Allah ziwe juu yake: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, siku moja nikawa karibu naye tukiwa...
Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa anapolala kitandani kwake wak...
Ilikuwa katika miongozo yake Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- pindi anapopanda kitandani kwake kwa ajili ya kulala, ni kukusanya viganja vyake na...
Kutoka kwa Shadaad Bin Ausi Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Bwana wa Istighfari (Dua y...
Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaeleza kuwa Istighfari (Kuomba msamaha) kuna matamshi mengi, nakuwa matamshi bora na makubwa zaidi ni mja kusema...

Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Ilikuwa Dua aiombayo zaidi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:ni "Ewe Mola wetu Mlezi, tupe duniani mazuri, na Akhera mazuri, na utukinge na adhabu ya moto".

Kutoka kwa Abuu Dardaa -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Je, nisiwaambieni matendo bora zaidi kwenu, na masafi zaidi mbele ya Mfalme wenu, na yatakayo kunyanyueni juu zaidi katika daraja zenu, na bora kwenu kuliko kutoa dhahabu na pesa, na bora kwenu kuliko hata kukutana na adui yenu na mkapiga shingo zao na wakapiga shingo zenu?" Wakasema: Ndiyo. Akasema: “Ni kumtaja Mwenyezi Mungu".

Kutoka kwa Muadhi bin Jabali -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, nikajikuta siku moja niko karibu naye tukiwa tunatembea, nikasema: Ewe Mtume wa Allah nieleze ibada ambayo nikiifanya itaniingiza peponi, na itaniweka mbali na moto, akamjibu: "Umeniuliza kuhusu jambo kubwa, lakini nijepesi kwa yule atakayefanyiwa wepesi na Mwenyezi Mungu Mtukufu: ni kumuabudu Mwenyezi Mungu bila kumshirikisha na chochote, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani, na kuhiji. kisha akasema Mtume: Je, nikujulishe milango ya kheri? Funga ni kinga, na sadaka inaondosha madhambi kama maji yanavyo uzima moto, na swala ya mtu katikati ya usiku, kisha akasoma kauli ya Mwenyezi Mungu: "Mbavu zao zinaachana na vitanda..." mpaka alipo fikia mwisho wa aya "wanao jua". Kisha akasema Mtume: Je nikueleze kichwa cha mambo yote na nguzo yake na kilele chake? nikajibu ndio ewe mjumbe wa Allah, akasema: Kichwa cha mambo yote ni Uislam, na nguzo yake ni Swala, na kilele chake ni Jihadi. kisha akasema: Je nikujulishe kinacho yahifadhi na kuyatunza matendo hayo? nikasema ndio ewe Mtume wa Allah, akaushika ulimi wake kisha akasema: uzuwie ulimi wako, nikamuuliza: Ewe Mtume wa Allah je tutahesabiwa kwa kila tunacho kizungumza? Akasema: akukose mamako, hakuna kitakacho waingiza watu wengi motoni kama chumo za ndimi zao".

Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa anapolala kitandani kwake wakati wa kila usiku alikuwa akikusanya viganja vyake, kisha akivipuliza na kuvisomea : {Qul-huwallahu Ahad}, na {Qul-A uudhu birabbil falaq} na (Qul-Auudhu birabbi naas } Kisha hujipaka kwa viganja hivyo sehemu awezayo katika mwili wake, anaanza kupaka kichwa chake na uso wake na sehemu ya mbele ya mwili wake, anafanya hivyo mara tatu.

Kutoka kwa Shadaad Bin Ausi Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Bwana wa Istighfari (Dua ya kuomba msamaha) Ni kusema: Allaahumma anta Rabbi Laa ilaaha illaa anta, khalaqtani wa anaa abduka wa ana a'laa a'hdika, wawa'dika mastatwa'tu, auudhubika min Sharri maa swana'tu, abuu ulaka bini'matika alaiyya, wa abuu ulaka bidhambi faghfirlii, fa innahuu laa yaghfirudh-dhunuuba illaa anta" Akasema: "Na atakayeisema dua hii mchana akiwa na yakini nayo, akafa katika mchana wake huo kabla hajafika jioni, basi atakuwa miongoni mwa watu wa peponi, na atakayeisema wakati wa usiku akiwa na yakini nayo, akafariki kabla hajafika asubuhi, basi huyo atakuwa miongoni mwa watu peponi".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: Yakwamba yeye alikuwa akisema anapoamka: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeamka, na kwako tunashinda, na kwako tunakuwa hai, na kwako tutakufa, na kwako tutafufuliwa" Na anaposhinda jioni anasema: "Kwako tumeshinda, na kwako tumeamka, na kwako tunakuwa hai, na kwako tunakufa, na kwako tutafufuliwa" Akasema: Na mara nyingine: "Na kwako ndio marejeo".

Kutoka kwa Abana bin Othman amesema: Nilimsikia Othman bin Affan radhi za Allah ziwe juu yake akisema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Yeyote atakayesema: Bismillaahi lladhi laa yadhurru ma'asmihi shai un fil Ardhwi walaa fis samaai, wahuwas samiiu'l 'aliim, (Kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye hakuna kinachoweza kudhuru pamoja na jina lake kitu chochote ardhini wala mbinguni, naye ni msikivu na mjuzi) mara tatu, basi halitomfika balaa la ghafla, mpaka atakapoamka, na atakayesema wakati wa asubuhi mara tatu, halitomfika balaa la ghafla mpaka atakapofika jioni" Akasema: Akapatwa na mtihani Abana bin Othman Al-Faaliji, basi yule bwana aliyesikia hadithi akawa anamtazama, akasema kumwambia: Vipi mbona unanitazama? Wallahi sijamsemea uongo Othman, wala Othman hajamsemea uongo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, lakini siku niliyofikwa na balaa, nilichukizwa na jambo fulani nikasahau kuisoma.

Kutoka kwa Abdillah Bin Khubaibi Radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye amesema: Tulitoka katika usiku wa mvua kubwa na giza nene, tukimtafuta Mtume rehema na amani ziwe juu yake; ili atusalishe, anasema: Nikampata, akasema: "Sema" Nikawa sikusema kitu, kisha akasema: "Sema", Nikawa sikusema kitu, akasema: "Sema" Nikasema: Niseme nini? Akasema: "Sema Yeye ni Mwenyezi Mungu mmoja tu" na sura mbili za kinga unapofika nyakati za jioni na nyakati za asubuhi mara tatu, zitakutosheleza kila kitu".

Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Siku moja nyakati za usiku nilimkosa kitandani Mtume rehema na amani ziwe juu yake nikaanza kumtafuta ukaangukia mkono wangu ndani ya nyayo zake zikiwa zimesimamishwa akiwa ndani ya msikiti, huku akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu ninajilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako, na salama yako dhidi ya adhabu zako, na ninajilinda kwako kutokana nawe, siwezi kuzidhibiti sifa zako kwa idadi maalum kama ambavyo wewe ulivyoisifu nafsi yako"

Imepokewa kutoka kwa Jundubi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Maneno yanayopendeka zaidi kwa Allah ni manne: Sub-haanallah, Al-hamdulillaah, na Laa ilaaha illa llaah, na Allahu Akbar, haidhuru ikiwa utaanza na lolote kati ya hao".

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Ayub -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayesema: Laa ilaaha illa llaahu wahdahu Laa shariika lahu, Lahul-Mulku walahul hamdu Wahuwa a'laa kulli shai-in qadiir, mara kumi (10) atakuwa ni kama aliyewaacha huru watu wanne katika wana wa Ismail".

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Maneno mawili mepesi mno katika ulimi, ni mazito mno katika mizani, yanapendeka mno kwa Al-Rahmani (Mwingi wa rehema) Ni: Sub-haanallahil Adhwiim, Sub-haanallaahi wabihamdihi".