Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Fanyeni matendo na muwe na...
Anahimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba kufanya amali njema, na wamche Mwenyezi Mungu kadiri wawezavyo, pasina kuchupa mipaka wala uze...
Kutoka kwa bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakuacha Jibrili kunius...
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Jibrili akikariri kwake na akimuamrisha kumjali jirani, ambaye ni wakaribu kimakazi, sawa awe muis...
Imepokewa kutoka kwa Abuu Dardaa -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayeitetea heshima ya nd...
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayeitetea heshima ya ndugu yake muislamu akiwa hayupo (katika mazungumzo) kwa kukataza watu ku...
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hawezi kuwa na imani mmoja wenu...
Amebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa imani kamili ya Muislamu yeyote haikamiliki mpaka ampendelee nduguye anachokipenda yeye, kat...
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe kwake- mke wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anasimulia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-...
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa upole na ulaini na utaratibu katika kauli na matendo huyazidishia mambo uzuri na ukamilifu na...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Fanyeni matendo na muwe na msimamo, na tambueni kuwa hatosalimika mmoja wenu kwa sababu ya matendo yake, wakasema: Hata wewe ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?! Akasema: Hata mimi isipokuwa atakaponifunika mimi Mwenyezi Mungu kwa huruma zake na fadhila zake".

Kutoka kwa bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakuacha Jibrili kuniusia kuhusu jirani, mpaka nikadhania kuwa atamrithisha".

Imepokewa kutoka kwa Abuu Dardaa -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayeitetea heshima ya ndugu yake basi Mwenyezi Mungu ataukinga uso wake na moto siku ya Kiyama".

Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hawezi kuwa na imani mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake anachokipenda yeye katika nafsi yake".

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe kwake- mke wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anasimulia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alisema: "Hakika upole hauwi ndani ya kitu isipokuwa hukipendezesha, na hautolewi ndani ya kitu ila hukichafua".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika dini ni nyepesi, na hatoifanyia mkazo dini yeyote ila itamshinda, basi shikamaneni na mfanye kadiri ya uwezo yanayoweza kukuwekeni karibu, na toeni bishara, na takeni msaada nyakati za asubuhi au mchana au sehemu ya usiku"

Kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Fanyeni mambo kuwa mepesi na wala msiyafanye kuwa magumu, na wapeni watu bishara njema na wala msiwakimbize".

Imepokewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Tulikuwa kwa Omari akasema: "Tumekatazwa kujilazimisha".

Na imepokewa kutoka kwa bin Omari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake - amesema: "Atakapo kula mmoja wenu basi na ale kwa mkono wake wa kulia, na atakapo kunywa basi na anywe kwa mkono wake wa kulia, kwani Shetani anakula kwa mkono wake wa kushoto, na anakunywa kwa mkono wake wa kushoto".

Kutoka kwa Omari bin Abii Salama -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa kijana mdogo ndani ya nyumba ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na mkono wangu ulikuwa ukizunguka huku na kule katika sahani (ya chakula), akasema kuniambia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: " Ewe kijana, mtaje Mwenyezi Mungu, na kula kwa mkono wako wa kulia, na kula kile kinachokuelekea" Ulibakia kuwa ndio ulaji wangu huo hata baada yake.

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Allah humridhia mja anapokula chakula akamshukuru juu ya chakula hicho, au akanywa kinywaji chochote akamshukuru kwa kinywaji hicho".

Kutoka kwa Salama bin Al Ak'wa'i -Radhi za Allah ziwe juu yake. Amesimulia kuwa mtu mmoja alikula chakula kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kwa mkono wake wa kushoto, akasema: "Kula kwa mkono wako wa kulia", Akasema: Siwezi, akasema: "Kamwe, hutoweza!", Hakuna kilichomzuia ila ni kiburi, akasema: hakuweza tena kuunyanyua kwenda kinywani kwake.