Imepokelewa kutoka kwa Jaabir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msijifunze elimu kwa ajili y...
Ametahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutafuta elimu kwa lengo la kujifaharisha kuwa naye ni katika Maulamaa, na kujitangaza kuwa mimi...
Imepokewa kutoka kwa Othman -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mmbora wenu ni yule aliyejifunza...
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa muislamu bora na aliye na daraja ya juu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu: Ni yule aliyejifunza Qur'...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Abdulrahman Al-Sulamiy- Mwenyezi Mungu amrehemu amesema: Ametusimulia mmoja miongoni mwa waliokuwa wakitusomea Qur'ani kat...
Walikuwa Maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- wakipokea Aya kumi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na hawakuwa wakihama kwe...
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayesoma herufi moja...
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila muislamu anayesoma herufi moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu basi atapata jema moja kwa he...
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu ya...
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa msomaji wa Qur'ani mwenye kufanyia kazi yaliyomo ndani yake, aliyeshikamana na kuisoma na kuihifad...

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msijifunze elimu kwa ajili ya kujifaharisha kuwa ni katika maulama, wala kwa kujadiliana na wasiokuwa na elimu, wala kuonekana ni mtu bora kwenye vikao, na yeyote atakaye fanya hivyo basi anastahiki kuingia motoni."

Imepokewa kutoka kwa Othman -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mmbora wenu ni yule aliyejifunza Qur'ani na akaifundisha".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Abdulrahman Al-Sulamiy- Mwenyezi Mungu amrehemu amesema: Ametusimulia mmoja miongoni mwa waliokuwa wakitusomea Qur'ani katika Maswahaba wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- walikuwa wakitusomea Aya kumi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hivyo hawakuwa wakichukua Aya kumi zingine mpaka wawe wamekwishayafanyia kazi yaliyo ndani ya aya hizo kumi kwa kujifunza na kuyafanyia kazi, wakasema: Basi tukajifunza elimu na kuifanyia kazi.

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allah basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na jema hilo hulipwa mara kumi mfano wake, sisemi (Alif Laam Miim) ni herufi, lakini (Alif) ni herufi, na (Laam) ni herufi, na (Miim) ni herufi".

Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ataambiwa msomaji wa Qur'ani: Soma na upande daraja, na soma kwa utulivu kama ulivyokuwa ukisoma Duniani, kwa hakika upandaji wa cheo chako utakomea katika Aya ya mwisho utakayoisoma."

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Je anapenda mmoja wenu pindi atakaporudi kwa mke wake apate Ngamia watatu wenye mimba na walio nenepa?" Tukasema: Ndiy. Akasema: "Basi aya tatu anazozisoma mmoja wenu katika sala zake ni bora kwake kuliko Ngamia watatu wenye mimba na walionenepa."

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash'ary-Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Shikamaneni vizuri na hii Qur'ani, namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hutoroka kwa kasi mno kuliko hata Ngamia katika kamba yake".

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, hakika Shetani hukimbia kutoka katika nyumba inayosomwa suratul Baqara ndani yake".

Imepokelewa kutoka kwa Ubaiyya bin Kaab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ewe baba Mundhir, hivi unaijua aya gani katika kitabu cha Mwenyezi Mungu ambayo ni tukufu zaidi kwako?" Akasema: Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wajuzi zaidi. Akasema: "Ewe baba Mundhir, hivi unaijua aya gani katika kitabu cha Mwenyezi Mungu ambayo ni tukufu zaidi?" Akasema: Nikasema: {Allahu laa ilaaha illa huwal hayyul qayyuum} Al-baqara: Basi akanipiga katika kifua changu, akasema: Nakuombea Mwenyezi Mungu elimu ikupe furaha ewe baba Mundhir."

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayesoma aya mbili za mwisho wa suratul Baqara zitamtosheleza".

Kutoka kwa Abuu Dardai radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayehifadhi aya kumi za mwanzo wa suratul Kahf, atakingwa na Dajali". Na katika riwaya nyingine: "Za mwisho wa suratul Kahf".

Imepokewa Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Dua ndio ibada", Kisha akasoma: "Na amesema Mola wenu Mlezi niombeni mimi nitakujibuni, hakika wale wanaofanya kiburi katika ibada yangu wataingia Jahannam wakiwa madhalili" [Ghafir: 60].