- Kumependekezwa kuzidisha ibada na swala za sunna ndani ya majumba.
- Haifai kuswali makaburini; kwa sababu ni njia katika njia za shirki na kuwakweza wafu, isipokuwa swala ya jeneza.
- Katazo la kuswali makaburini limethibiti kwa Masahaba, na kwa sababu hiyo amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nyumba kufanywa mfano wa makaburi hakuswaliwi ndani yake.