- Dua ndio asili ya ibada na wala haifai kuilekeza kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu.
- Dua inaambatana na uhalisia wa kuabudu na kukiri utajiri wa Mola Mlezi na uwezo wake Yeye Mtukufu, na uhitaji wa mja kwake.
- Kemeo kali likiwa ni malipo ya kiburi cha kutomuabudu Mwenyezi Mungu na kuacha kumuomba, nakwamba wale wanaofanya jeuri kumuomba Allah wataingia katika Jahannam wakiwa wanyonge madhalili.