- Kumebainishwa fadhila ya suratul Kahaf, na kuwa mwanzo wake na mwisho wake zinakinga na fitina za Dajali.
- Kumeelezwa swala la Dajali, na kumebainishwa yanayokinga na fitina hiyo.
- Himizo la kuihifadhi suratul Kahaf nzima, ikiwa atashindwa basi ahifadhi aya kumi za mwanzo na za mwisho.
- Amesema Al-Qurtubi katika sababu ya hilo: Imesemekana: Kwa sababu ya yale yaliyoko ndani ya kisa cha watu wa pangoni katika maajabu na miujiza, atakayeizingatia hatoshangazwa na jambo la Dajali na halitamtisha hilo na wala hatofitinika, na imesemekana: Kwa sababu ya kauli yake Mtukufu: "Ili kitoe onyo kali kutoka kwake" Kwa kuuhusisha ugumu na ukali na kwake, na ndio unafaa kwa yale atakayokuwa nayo Dajali katika kudai uungu na kutawala kwake na ukubwa wa fitina yake, inakuwa maana ya hadithi nikuwa: atakayesoma aya hizi na akazizingatia na akasimama katika maana zake zitamtahadharisha na atasalimika naye.