- Kumewekwa wazi ubora wa kuisoma Qur'ani ndani ya sala.
- Matendo mema ni bora na ni yenye kubakia kuliko starehe za Dunia zenye kuisha.
- Fadhila hizi haziishii tu kwa kusoma Aya tatu, bali kila msomaji anapozidi kusoma Aya nyingi za Qur'ani katika sala zake, malipo yake yanakuwa ni bora kwake kuliko idadi ya Ngamia wanene wenye mimba.