Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Kiapo hutoa bid...
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuapa na kukithirisha kiapo hata kama mtu akiwa mkweli katika kuuza na kununua, na akaeleza kuwa n...
Imepokewa kutoka kwa Bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Punguzeni...
Anaamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kupunguza sharubu na zisiachwe bali zipunguzwe, na azidi kupunguza zaidi. Na pamoja na hilo anaamr...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Asiangalie mwanaum...
Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwanaume kutazama uchi wa mwanaume mwenzie, au mwanamke kutazama uchi wa mwanamke mwenzie. Uchi: Ni k...
Kutoka kwa Abdallah bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake- amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hakuwa na maneo machafu wala m...
Haikuwa katika tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa na maneno machafu, au vitendo vibaya, na hakuwa anayataka hayo wala kuyatafuta kwa...
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika muumini hufikia kwa sababu...
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa tabia njema humfikisha mwenye tabia hiyo nafasi ya mwenye kufunga mchana daima na kusimama usik...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Kiapo hutoa bidhaa, na hufuta faida".

Imepokewa kutoka kwa Bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Punguzeni sharubu na mfuge ndevu".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Asiangalie mwanaume katika uchi wa mwanaume mwenzie, wala mwanamke kutazama uchi wa mwanamke mwenzie, na wala asijifunike mwanaume na mwanaume mwenzie shuka moja, na wala mwanamke asijifunike na mwanamke mwenzie shuka moja".

Kutoka kwa Abdallah bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake- amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hakuwa na maneo machafu wala mwenye kuyatafuta, na alikuwa akisema: "Hakika katika wabora wenu ni mtu mwenye tabia njema kuliko wote".

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika muumini hufikia kwa sababu ya tabia zake njema daraja ya mfungaji mwenye kusimama usiku".

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Muumini iliyekamilika zaidi imani yake ni yule mwenye tabia nzuri zaidi kuliko wengine, na mbora wenu ni yule mbora wenu kwa wake zake".

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: "Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo yatakayowaingiza watu peponi kwa wingi, akasema: "Ni uchamungu na tabia njema", na akaulizwa kuhusu mambo yatakayowaingiza watu motoni kwa wingi akasema: "Mdomo na utupu".

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mtu mwenye tabia nzuri mno kuliko watu wote.

Amesema Sa'd bin Hisham bin Aamiri -alipoingia kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake: Ewe mama wa waumini, nieleze kuhusu tabia ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akasema: Hivi si unasoma Qur'ani? Nikasema: Ndiyo! akasema: Basi tabia ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ilikuwa ni Qur'ani.

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendezwa sana na kuanzia kulia, katika kuvaa kwake viatu, na kutana kwake nywele, na twahara yake, na katika mambo yake yote.

Imepokewa Kutoka kwa Shaddad bin Ausi -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Mambo mawili niliyahifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alisema: "Hakika Mwenyezi Mungu amewajibisha (kufanya) wema katika kila kitu, mtakapoua basi ueni kwa namna iliyokuwa nzuri, na mtakapochinja basi kwa namna iliyokuwa nzuri, na anoe mmoja wenu zana yake ya kuchinjia, na akistareheshe kichinjwa chake".

Imepokewa kutoka kwa Abdullahi bin Amry -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika waadilifu mbele ya Mwenyezi Mungu watakuwa katika mimbari za nuru, kuliani mwa Allah Mtukufu, na mikono yake yote miwili ni kulia , wale wanaofanya uadilifu katika hukumu zao na familia zao, na vile wanavyovitawala"