Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mtu mwenye tabia nzuri mno kuliko watu wote
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mtu mwenye tabia nzuri mno kuliko watu wote.
Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Ufafanuzi
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa na tabia zilizokamilika kuliko watu wote, na mtu wa mbele katika tabia njema na mambo mazuri, kama maneno mazuri, na kufanya heri, na uso mkunjufu, na kujizuia na maudhi na kuyavumilia kutoka kwa wengine.
Hadeeth benefits
Ukamilifu wa tabia ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yeye ndiye kiigizo kamili katika tabia nzuri.
Himizo la kuiga kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika tabia nzuri.
Share
Use the QR code to easily share the message of Islam with others