- Katazo la kutazama uchi, isipokuwa mume na mke wake.
- Hima ya Uislamu juu kuisafisha jamii, na kufunga njia zinazopelekea katika machafu.
- Inaruhusiwa kuangalia uchi kukiwa na haja ya kufanya hivyo, kama matibabu na mfano wake, na isiwe kwa matamanio.
- Muislamu ameamrishwa kusitiri uchi wake na kuinamisha macho yake kutotazama uchi wa mwenzie.
- Kumetajwa pekee wanaume kuwatazama wanaume wenzao na wanawake kuwatazama wanawake wenzao; kwa sababu ndio kishawishi kikubwa katika kutazama na kufunua uchi.