- Ni lazima kwa muumini ajiweke mbali na maneno machafu na vitendo vibaya.
- Ukamilifu wa tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hayatokei kwake ila matendo mema na maneno mazuri.
- Tabia njema ni uwanja wa mashindano, atakayeshinda atakuwa ni muumini bora na mwenye imani iliyokamilika zaidi kuliko wote.