Kutoka kwa Jubairi bin Mutwim -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Haingii peponi mk...
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakayewakatia ndugu zake wa karibu zile haki za wajibu kwao, au akawaudhi au kuwafanyia ubaya,...
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- : Yakwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake Amesema: "Atakay...
Anahimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya kuwaunga ndugu wa karibu kwa kuwatembelea na takrima za mwili na mali na mengineyo, nakuwa kufa...
Imepokelewa Kutoka kwa Abdillah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Muunga udugu s...
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Kuwa mwanadamu kamili katika kuunga udugu na kuwatendea wema ndugu wa karibu si yule mtu mwenye kulipa...
Kutoka kwa Bahzi bin Hakim kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani nimfanyie wema zaidi? Ak...
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mtu muhimu zaidi kufanyiwa wema kuliko wote, na kumfanyia hisani, na kuamiliana naye vizuri, na k...
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hivi mnajua ni nini kusengeny...
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ukweli kuhusu kusengenya kuliko haramishwa, nako ni: Kumsema muislamu asiyekuwepo kwa yale anayoyach...

Kutoka kwa Jubairi bin Mutwim -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Haingii peponi mkata udugu".

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- : Yakwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake Amesema: "Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na acheleweshewe ajali yake, basi na aunge udugu wake".

Imepokelewa Kutoka kwa Abdillah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Muunga udugu si mlipa fadhila, bali muunga udugu ni yule ambaye udugu wake ukikatwa anauunga".

Kutoka kwa Bahzi bin Hakim kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani nimfanyie wema zaidi? Akasema: "Mama yako, kisha mama yako kisha mama yako, kisha baba yako, kisha anayefuata kwa ukaribu kisha anayemfuata kwa ukaribu".

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hivi mnajua ni nini kusengenya?", Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi, akasema: "Ni kumsema ndugu yako kwa yale anayoyachukia", Pakasemwa: Waonaje ikiwa niyasemayo yako kwa ndugu yangu? Akasema: "Yakiwa kwake uyasemayo utakuwa umemsengenya, na ikiwa hana basi utakuwa umemzulia uongo".

kutoka kwa bin Omar -Radhi za Allah ziwe juu yao- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- "kila kilevi ni haramu, na atakayekunywa pombe duniani na akafa akiwa mlevi kupindukia na hakutubia, hatoinywa huko akhera"

Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake alisema: "Amemlaani Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake- mtoa rushwa na mpokea rushwa katika hukumu".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: " Msihusudiane, na wala msipandishiane bei, na wala msichukiane, na wala msitengane, na wala wasiuze baadhi yenu juu ya biashara ya wengine, na kuweni waja wa Mwenyezi Mungu ndugu muislamu ni ndugu wa muislamu, asimdhulumu, na wala asimsaliti, na wala asimdharau, ucha Mungu uko hapa" Na huku akiashiria katika kifua chake mara tatu "Yamtosha mtu kuwa ni shari kwake kwa kumdharau ndugu yake muislamu, kila muislamu kwa muislamu mwenzake ni haramu damu yake, na mali yake, na heshima yake".

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Tahadharini na dhana; kwani dhana ni mazungumzo ya uongo mno, na wala msitiliane shaka (kwa kuhisiana vibaya), na wala msichunguzane, na wala msihusudiane, na wala msitengane, na wala msichukiane, na kuweni waja wa Mwenyezi Mungu ndugu wamoja"

Imepokewa kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Haingii peponi mfitinishaji".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Umma wangu wote unasamehewa isipokuwa wenye kutangaza wazi madhambi, na hakika miongoni mwa kutangaza machafu, ni mtu kutenda dhambi usiku, kisha akaamka akiwa kasitiriwa na Mwenyezi Mungu juu ya dhambi hilo, akaanza kusema: We fulani, jana usiku mimi nilifanya kadhaa wa kadhaa, hali yakuwa alilala usiku kucha Mola wake Mlezi akimsitiri, kisha anaamka asubuhi anafunua pazia la Mwenyezi Mungu".

Na kutoka kwa Ibn Omari Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake: Ya kwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwahutubia watu siku ya ufunguzi wa mji wa Makka, akasema: "Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ameondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga, na kujifaharisha kwa nasaba , basi watu wako aina mbili: Mwema mchamungu mtukufu kwa Mwenyezi Mungu, na muovu mbaya dhalili kwa Mwenyezi Mungu, na watu wote ni wana wa Adam, na amemuumba Mwenyezi Mungu Adam kutokana na udongo. Amesema Mwenyezi Mungu: "Enyi watu hakika sisi tumekuumbeni kutokana na mwanaume na mwanamke na tukakufanyeni kuwa mataifa na makabila tofauti tofauti, ili mfahamiane, hakika mbora wenu kwa Mwenyezi Mungu ni mchamungu wenu, hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi na ana habari (za mambo yote)" [Al Hujuraat: 13].