Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-: "Nikuwa Talbiya (kuitika) kwa Mtume rehema na amani ziwe juu ya...
Zilikuwa talbiya (kuitika katika Hija) kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kuingia katika ibada ya Hija au Umra ni kusema: "Nimekuitikia...
Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao na baba yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu...
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa amali njema ndani ya siku kumi za mwanzo wa mwezi Dhul-Hija ni bora kuliko siku zingine. Mas...
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Wapigeni vita washirikina kwa ma...
Aliamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwapiga vita makafiri, na kutumia juhudi katika kukabiliana nao kwa kila nyenzo kwa kadri iwezekanavyo...
Kutoka kwa Abul Hauraai Assa'di amesema: Nilisema kumwambia Hassan bin Ally radhi za Allah ziwe juu yao: Ulihifadhi nini kutoka kwa Mtume rehema na am...
Aliamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuacha kile ulicho na shaka nacho katika maneno na matendo nakuwa jambo hilo limekatazwa toka mwanzo, j...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu am...
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Muislamu haadhibiwi kwa mazungumzo ya shari ya nafsi yake kabla ya kuyafanyia kazi au kuyazungumza,...

Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-: "Nikuwa Talbiya (kuitika) kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kulikuwa ni: Labbaikallaahumma labbaika -Nimekuitikia ewe Mola nimekutikia, Labbaika laa shariika laka labbaika -Nimekuitikia huna mshirika wako nimekuitikia, Hakika sifa njema na neema zote ni zako pamoja na ufalme, wewe pekee usiye na mshirika.". Amesema: Na alikuwa Abdallah bin Omari akizidisha ndani yake: "Labbaika Labbaika wasa'daika, -Nimekuitikia nimekuitikia na utukufu ni wako, wal khairu biyadaika, -Na heri iko mikono mwako, na hamu zote na matendo mwisho ni kwako".

Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao na baba yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakuna siku ambazo matendo mema yanapendeka zaidi ndani yake kwa Mwenyezi mungu kuliko siku hizi" Yaani: Siku kumi (za mwanzo wa Dhul-Hija), Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hata kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Akasema: "Hata kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa mtu aliyetoka kwa nafsi yake na mali yake na hakurudi na chochote katika hivyo".

Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Wapigeni vita washirikina kwa mali zenu na nafsi zenu na ndimi zenu".

Kutoka kwa Abul Hauraai Assa'di amesema: Nilisema kumwambia Hassan bin Ally radhi za Allah ziwe juu yao: Ulihifadhi nini kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake? Akasema: Nilihifadhi kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake? "Acha linalokutia shaka fanya lisilokutia shaka, kwani ukweli ni utulivu, na bila shaka uongo ni shaka"

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu amewafutia umma wangu yale yanayozungumzwa na nafsi zao, madamu hayajafanyiwa kazi au kuzungumzwa".

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu hatazami sura zenu na mali zenu, lakini anatazama katika nyoyo zenu na matendo yenu."

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -sala na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu hupata wivu, na hakika muumini hupata wivu, na wivu wa Mwenyezi Mungu ni pale muumini anapoyafanya yale aliyomharamishia juu yake".

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Yaepukeni mambo saba yenye kuangamiza" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yapi hayo? Akasema: "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu (na kitu kingine), na uchawi, na kuua nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa haki, na kula riba, na kula mali ya yatima, na kukimbia siku ya vita, na kuwatuhumu machafu waumini wa kike waliojihifadhi wasiojua lolote (kuhusu huo uchafu)"

Imepokewa kutoka kwa Abuu Bakra -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?" Kalisema hilo mara tatu, wakasema: Tueleze ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu (na kitu kingine), na kuwaasi wazazi wawili" Na akakaa vizuri na alikuwa kaegemea, akasema: "Fahamuni, na kusema uongo", akasema: Akaendelea kulikariri neno hilo mpaka tukasema: Laiti angenyamaza.

Imepokewa kutoka kwa Abdillah Ibn Amri bin Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Madhambi makubwa: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kuwaasi wazazi wawili, na kuuwa nafsi, na kiapo cha uongo".

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "La kwanza litakalohukumiwa kati ya watu siku ya kiyama ni katika damu".

Imepokewa Kutoka kwa Abdillah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Atakayemuua aliyechukua ahadi ya kulindwa, hatonusa harufu ya pepo, na hakika hurufu yake hupatikana kuanzia mwendo wa miaka arobaini".