- Kuwa na jukumu kubwa la kuirekebisha nafsi, na kuisafisha kutokana na kila sifa mbaya.
- Moyo hutengemaa kwa Ikhlaswi, na matendo hutengemaa kwa kumfuata Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na sehemu hizi mbili ndio mahali pa kutazamwa na kuzingatiwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Mwanadamu asidanganyike kwa mali yake wala kwa uzuri wake wala kwa mwili wake wala kwa chochote miongoni mwa mionekano ya dunia.
- Tahadhari ya kuridhika na mionekano, na kutorekebisha ndani ya moyo.