- Ubora wa matendo mema katika siku kumi za Dul-Hija, ni juu ya muislamu atumie fursa ya siku hizi na azidishe ibada ndani yake, kama kumtaja Allah Mtukufu, na kusoma Qur'ani, na takbiri (Allahu Akbar) na tahlil (Laa ilaaha illa llaah) na tahmidi (Alhamdulillaah), na swala na sadaka na swaumu, na amali zote njema.