- Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na Kutukuka, ameyaacha na kuyasamehe mawazo na fikira zinazojitokeza katika nafsi, mtu huzungumza mwenyewe ndani ya moyo wake na kupita katika mawazo yake.
- Mtu atakapofikiria talaka, na ikapita akilini mwake, lakini akawa hajaitamka na wala hajaiandika, basi hiyo haizingatiwi kuwa ni talaka.
- Mazungumzo ya nafsi mtu hahesabiwi vyovyote vile yatakavyokuwa makubwa madam hayajakita ndani ya nafsi yake na akayafanyia kazi au kuyazungumza.
- Ukubwa wa cheo cha umma wa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake kwa kufanywa maalum kwa kutokuadhibiwa kwa mazungumzo ya nafsi, kinyume na umma zilizokuwa kabla yetu.