- Himizo la kupigana Jihadi na washirikina kwa nafsi na mali na ulimi; kila mmoja kulingana na uwezo wake, nakuwa Jihadi haishii katika kukabiliana nao kwa nafsi pekee.
- Amri ya Jihadi ni ya wajibu, na inaweza kuwa wajibu kwa kila mtu, na inaweza kuwa wajibu kwa watu baadhi.
- Mwenyezi Mungu aliweka sheria ya Jihadi kwa mambo mengi, miongoni mwake: La kwanza: Kupambana na ushirikina na washirikina; kwa sababu Mwenyezi Mungu haukubali ushirikina milele, la pili: Kuondoa vikwazo vinavyojitokeza katika njia ya ujumbe wa Mwenyezi Mungu, la tatu: Kuihami itikadi sahihi dhidi ya yote yaliyokinyume nayo, la nne: Kuwalinda waislamu na nchi zao na mali zao.