Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Amesema Mwenyezi Mungu Mtukuf...
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Toa ewe mwanadamu -katika matumizi ya wajibu na ya hiyari- nikuk...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapotoa matumizi mtu k...
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakapotoa mtu matumizi kwa familia yake, wale anaolazimika kuwahudumia kama mke wake na watoto...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Anapo kufa mwanadamu maten...
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa amali za maiti hukatika kwa kufa kwake, hayapatikani mema tena baada ya kifo chake isipokuwa kwa mam...
Kutoka kwa Maliki bin Ausi bin Hadathani yakuwa yeye alisema: Niligeuka nikasema ni nani anayechenji pesa? Twalha bin Ubaidillah akasema wakati akiwa...
Taabii (Mwanafunzi wa Maswahaba) Malik bin Ausi anaeleza kuwa alikuwa na dinari za dhahabu, na alitaka kuzibadilisha kwa dirham za fedha, basi Twalha...
Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Alifaradhisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fi...
Amewajibisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri baada ya Ramadhani, nayo kwa kiwango cha kibaba inafikia uzito wake machoto manne. Na...

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Toa ewe mwanadamu na mimi nikupe".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapotoa matumizi mtu kwa familia yake kwa kutaraji malipo, basi hiyo kwake ni sadaka".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Anapo kufa mwanadamu matendo yake hukatika isipokuwa mambo matatu: Sadaka yenye kuendelea, au elimu yenye manufaa, au mtoto mwema wa kumuombea dua"

Kutoka kwa Maliki bin Ausi bin Hadathani yakuwa yeye alisema: Niligeuka nikasema ni nani anayechenji pesa? Twalha bin Ubaidillah akasema wakati akiwa kwa Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yao wote: Tuonyeshe Dhahabu yako, kisha tuletee, atakapokuja mfanyakazi wetu tutakupa pesa yako, akasema Omari bin Khattwab: Hapana, ni lazima utampa haki yake, au umrejeshee Dhahabu yake, kwani Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Fedha kwa dhahabu ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na ngano isiyokobolewa ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na shairi (ngano iliyokobolewa ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na tende kwa tende ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono".

Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Alifaradhisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri kibaba cha tende, au kibaba cha ngano, kwa mtumwa na aliyehuru, na mwanaume na mwanamke, na mdogo na mkubwa katika waislamu, na akaamrisha itolewe kabla ya watu kutoka kwenda katika swala.

Kutoka kwa Abdullah bin Salam radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alipokuja Madina Mtume rehema na amani ziwe juu yake, watu walikusanyika mbele yake, pakasemwa: Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu, Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu, wakasema mara tatu, nikaja pamoja na watu kutazama, na nilipouona uso wake nikajua kuwa uso wake si uso wa muongo, kwa hivyo jambo la kwanza nililomsikia akizungumza alisema kuwa: "Enyi watu, toleaneni salamu na muunge udugu, na mlishe chakula, na msali usiku watu wakiwa wamelala, mtaingia peponi kwa amani".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha kwayo Manabii, akasema Allah Mtukufu: "Enyi Mitume! Kuleni katika vile vilivyo vizuri na mtende mema, hakika mimi kwa yale mnayoyafanya ni Mjuzi" [Al-Muuminuun: 51] Na akasema Allah Mtukufu: "Enyi mlioamini! Kuleni katika vizuri miongoni mwa vile tulivyokuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu ikiwa kweli nyinyi mnamuabudu yeye peke yake" [Al-baqara: 172] akasema: Kisha akataja tukio la mtu mmoja mwenye safari ndefu, nywele zake zimetimka, kajaa vumbi, ananyanyua mikono yake kuelekea mbinguni (anasema) Mola wangu Mola wangu! (wakati huo) chakula chake ni cha haramu, na mavazi yake ni ya haramu, na kinywaji chake ni cha haramu, na lishe yake yote ni ya haramu, itawezekana vipi kujibiwa kwa mtu kama huyo?!".

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayempa muda mwenye hali ngumu, au akamfutia deni, Allah atampa kivuli siku ya kiyama chini ya kivuli cha Arshi yake siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake."

Imepokelewa Kutoka kwa Jabiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Allah amhurumie mtu ambaye ni mpole anapouza, na anaponunua, na anapo dai deni".

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kulikuwa na mtu akiwakopesha watu,basi alikuwa akisema kumwambia kijana wake (Akienda kudai): Ukifika kwa mwenye hali ngumu, basi msamehe, huenda nasi Allah akatusamehe (alipokufa) akakutana na Allah, akamsamehe".

Kutoka kwa Khaula Al-Answariya -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika watu wanaotumia mali ya Mwenyezi Mungu pasina haki, hao (wana adhabu ya) moto siku ya Kiyama".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Amesema Mwenyezi Mungu: Kila amali ya mwanadamu hiyo ni ya kwake isipokuwa swaumu, bila shaka hiyo ni yangu na mimi ndiye ninayeilipa, na swaumu ni kinga, na itakapokuwa ni siku ya kufunga mmoja wenu basi asitamke machafu, wala asifanye fujo, na ikiwa kuna mtu atamtukana au akampiga, basi aseme, mimi nimefunga, namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hakika harufu ya mdomo wa mfungaji ni nzuri mno mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko harufu ya Miski, mfungaji anafuraha mbili anazofurahia: Anapofuturu hufurahi, na akikutana na Mola wake atafurahi kwa swaumu yake"