- Zakatul-fitiri ya Ramadhani ni lazima kutolewa kwa mtoto na mkubwa, na aliye huru na mamluki, na anasemeshwa hapa msimamizi na bosi, na anaitoa mwanaume kwa niaba yake na watoto wake na wale ambao ni wajibu kwake kuwahudumia.
- Si wajibu zakatul-fitiri kwa kichanga kilichoko tumboni, bali inapendeza tu.
- Kumebainishwa kinachotolewa katika zakatul-fitiri, nakuwa ni chakula cha watu walichokizoea.
- Uwajibu wa kuitoa kabla ya swala ya Iddi, na bora zaidi iwe asubuhi ya siku ya Iddi, na inafaa kuitoa kabla ya Iddi kwa siku moja au mbili.