Atakayempa muda mwenye hali ngumu, au akamfutia deni, Allah atampa kivuli siku ya kiyama chini ya kivuli cha Arshi yake siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayempa muda mwenye hali ngumu, au akamfutia deni, Allah atampa kivuli siku ya kiyama chini ya kivuli cha Arshi yake siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake."
Ufafanuzi
Ametueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayempa muda mdaiwa wake au akampunguzia katika deni lake, basi malipo yake: Nikuwa Allah atampa kivuli siku ya Kiyama ambayo jua litasogea karibu na vichwa vya waja na joto lake litakuwa kali mno, Hatopata yeyote kivuli isipokuwa atakayetiwa kivuli na Mwenyezi Mungu.
Hadeeth benefits
Fadhila za kuwafanyia wepesi waja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, nakuwa hilo ni katika sababu za kuokoka na misukosuko ya siku ya Kiyama.
Malipo huenda sawa na matendo.
Share
Use the QR code to easily share the message of Islam with others