- Kuna aina tano za vitu vilivyotajwa katika Hadith hii: dhahabu, fedha, ngano, shayiri, na tende Ikiwa uuzaji utafanyika katika kundi moja, masharti mawili lazima yatimizwe kwa ajili ya uhalali wake: kubadilishana katika kikao cha mkataba, na kufanana katika aina na uzito, kama vile dhahabu kwa dhahabu, vinginevyo itakuwa ni riba ya mkopo, na ikiwa ni tofauti mnavyouziana kama vile fedha na ngano kwa mfano, basi ili kusihi biashara hii linahitajika sharti moja wakati wa mkataba, vinginevyo itakuwa ni riba ya mkopo.
- Makusudio ya kikao cha makubaliano: Ni mahala pa kuuziana, sawa sawa wawe wamekaa au wanatembea, au wamepanda, na makusudio ya kuachana ni kila namna ya kuachana waliyoizoea watu.
- Katazo katika Hadithi linakusanya aina zote za dhahabu zilizosafishwa na ambazo hazijasafishwa, na aina zote za fedha, zilizosafishwa na zinginezo.
- Miamala ya kifedha ya zama hizi ni wajibu kufanyika kilichowajibu katika biashara ya dhahabu na fedha, yaani endapo utataka kubadili fedha ya noti au sarafu kwa fedha nyingine ya noti au sarafu, kama Riyal kwa Dirham au Shilingi kwa Dollar, hapa inajuzu kupishana thamani kwa namna watakavyoelewana pande zote mbili, lakini ni wajibu kukabidhiana katika kikao cha mauziano, vinginevyo mauziano yatakuwa batili, na muamala huu utakuwa umeingia katika Riba iliyoharamishwa.
- Miamala yote ya riba haifai, na makubaliano yake ni batili hata kama wataridhiana pande zote mbili; kwa sababu Uislamu unahifadhi haki ya mtu na ya Jamii nzima kwa ujumla, hata kama yeye mwenyewe atakubali haki yake iende.
- Kukataza uovu na kuuzuia kwa atakayeweza kulifanya hilo.
- Kutaja ushahidi wakati wa kukemea uovu, kama ilivyotokea kwa Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake.