Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Mimi nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakuna swala chakula kinapoku...
Amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuswali kinapotengwa chakula kile anachokitamani mwenye kuswali, na moyo wake umefungamana nacho....
Kutoka kwa Othman bin Abil Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yake-: Yakwamba yeye alimwendea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa...
Alikuja Othman bin Abil Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yake- kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika She...
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwizi mbaya zaidi kuliko watu wote, ni...
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwizi mbaya zaidi kuliko wote ni yule anayeiba swala yake; na hii ni kwakuwa; kuchukua mali ya...
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hivi haogopi mmoja wenu...
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ahadi ya adhabu kali kwa mwenye kunyanyua kichwa chake kabla ya imamu wake, kuwa Mwenyezi Mungu kuki...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khuduriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapo...
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ikiwa mwenye kuswali atasita katika swala yake na akashindwa kujua ameswali rakaa ngapi, tatu au nne...

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Mimi nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakuna swala chakula kinapokuwa tayari, na wala hakuna (swala) akiwa anazuia na kubana vichafu viwili(Haja kubwa na ndogo)".

Kutoka kwa Othman bin Abil Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yake-: Yakwamba yeye alimwendea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika shetani amekaa kati yangu na swala yangu na kisomo changu ananichanganya, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Huyo ni Shetani anaitwa Khinzab, ukimuhisi basi haraka sana taka ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yake, na uteme kushotoni kwako mara tatu", anasema: Nikafanya hivyo Mwenyezi Mungu akamuondosha kwangu.

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwizi mbaya zaidi kuliko watu wote, ni yule anayeiba swala yake" Akasema: Ataiba vipi swala yake? Akasema: "Hatimizi rukuu zake wala sijida zake".

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hivi haogopi mmoja wenu (Au: Hachelei mmoja wenu) atakapoinua kichwa chake kabla ya imamu, Mwenyezi Mungu akifanye kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye Mwenyezi Mungu sura yake kuwa sura ya punda".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khuduriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapopata shaka mmoja wenu katika swala yake, akawa hajui kaswali rakaa ngapi tatu au nne? Basi aachane na shaka na ajenge yakini (uhakika), kisha atasujudu sijida mbili kabla hajatoa salamu, ikiwa atakuwa kaswali rakaa tano basi zitamtetea katika swala yake, na kama aliswali kukamilisha nne; basi hiyo itakuwa ni kumvunja moyo shetani."

Kutoka kwa Waabiswa radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuona mtu mmoja akiswali peke yake nyuma ya safu, akamuamrisha arudie swala yake.

Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Masoud -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alitajwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mtu mmoja aliyelala usiku mpaka pakapambazuka, akasema: "Huyo ni mtu aliyekojolewa na Shetani ndani ya masikio yake, au alisema: ndani ya sikio lake".

Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Amesema: “Siku bora zaidi iliyochomozewa jua ni siku ya Ijumaa, ndani yake aliumbwa Adam, na ndani yake aliingizwa Peponi, na ndani ya siku hii akatolewa humo, na hakitosimama Kiyama ila siku ya Ijumaa".

Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakaye koga siku ya Ijumaa josho la janaba, kisha akatoka katika saa ya kwanza ni kana kwamba katoa sadaka ya ngamia, na atakayetoka katika saa ya pili ni kana kwamba katoa sadaka ya ng'ombe, na atakayetoka katika saa ya tatu ni kana kwamba katoa sadaka ya kondoo, na atakayetoka katika saa ya nne ni kana kwamba katoa sadaka ya kuku, na atakaye kwenda katika saa ya tano ni kama katoa yai, akitoka imamu Malaika wanahudhuria kusikiliza ukumbusho".

Kutoka kwa Thauban -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anapoondoka katika swala yake anaomba msamaha mara tatu, na anasema: "Allaahumma antas salaam waminkas salaam, tabaarakta yaa dhal-jalaali wal-ikraam", Anasema Walid: Nikasema kumwambia Auzaiy: Ni vipi unaomba msamaha: Akasema: Unasema: Astagh-firullaah, Astagh-firullaah.

Kutoka kwa Abuu Zubairi amesema: Alikuwa bin Zubairi akisema mwisho wa kila swala anapotoa salamu: "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul Mulku walahul-hamdu wahuwa a'laa kulli shai-in qadiir, Laa haula walaa quwwata illaa billaah, Laa ilaaha illa llaah, walaa na'budu illaa iyyaahu, Lahun-ni'matu walahul-fadhlu walahuth-thanaaul hasan, Laa ilaaha illa llaahu Mukhliswiina lahud-diina walau karihal kaafiruun" Na akasema: "Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitoa tahlil (Laa ilaaha illa llaah) kwa maneno haya mwisho wa kila swala".

Kutoka kwa Warraadi mwandishi wa Mughira amesema: Alinisomea Mughira bin Shu'ba katika kitabu kilichoandikwa kwenda kwa Muawia: Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikua akisema mwishoni mwa kila swala ya faradhi: "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul mulku walahul hamdu, wahuwa a'laa kulli shai in qadiir, Allaahumma laa maania limaa a'twaita walaa mu'twiya limaa mana'ta, walaa yanfa'u dhal jaddi minkal jaddu".