Kutoka kwa Buraida -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hakika a...
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ahadi na mkataba kati ya waislamu na wasiokuwa wao katika makafiri na wanafiki ni swala, atakay...
Imepokewa kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika kilicho...
Anatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuacha swala ya faradhi, na akaeleza kuwa kati ya mtu na baina ya kuingia katika shirki na ukafi...
Kutoka kwa Salim bin Abil Ja'di amesema: Mtu mmoja alisema: Laiti ningeswali nikastarehe, wakawa kana kwamba wamelitia dosari hilo, akasema: Nilimsiki...
Akasema mtu mmoja katika Masahaba: Laiti ningeliswali nikastarehe, waliokuwa naye waka kana kwamba wamemuabisha kwa hilo, akasema: Nilimsikia Mtume -R...
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapotoa takbira katika swala a...
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaposema “Allahu Akbar” kwa ajili ya swala, alikuwa akitulia kidogo kabla ya kusoma Al-Fatiha, ambamo ali...
Na kutoka kwa Ibn Omari Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake: Yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Alikuwa akinyanyua mikono yake usawa...
Mtume, rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akinyanyua mikono yake katika sehemu tatu wakati wa kuswali, usawa wa mabega ni: Pale panapounga kati ya...
Kutoka kwa Buraida -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hakika ahadi iliyopo kati yetu na wasiokuwa waislamu ni sala, na atakayeiacha sala basi huyo ni kafiri".
Imepokewa kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika kilicho kati ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha swala".
Kutoka kwa Salim bin Abil Ja'di amesema: Mtu mmoja alisema: Laiti ningeswali nikastarehe, wakawa kana kwamba wamelitia dosari hilo, akasema: Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Ewe Bilali, simamisha swala, tupe raha kwayo".
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapotoa takbira katika swala ananyamaza kidogo kabla hajaanza kusoma, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nimuweka fidia baba yangu na mama yangu, hebu nieleze kunyamaza kwako kati ya takbira na kisomo: Ni nini unasema: Akasema: Ninasema: Allaahumma baaid bainiy -Ewe Mwenyezi Mungu weka mbali baina yangu- wa baina khatwaayaaya -na baina ya makosa yangu- kamaa baa a'tta bainal mashriqi wal maghribi -kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi. Allaahumma naqqiniy- Ewe Mwenyezi Mungu nitakase mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- kamaa yunaqqath-thaubul abyadhwa -kama inavyotakaswa nguo nyeupe- minad danasi -kutokana na uchafu. Allaahumma ghsilniy -Ewe Mwenyezi Mungu nioshe mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- bil maai wath thalji wal baradi -kwa maji na barafu na baridi".
Na kutoka kwa Ibn Omari Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake: Yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Alikuwa akinyanyua mikono yake usawa wa mabega yake anapofungua swala, na anapotoa takbira ya kurukuu, na anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu anainyanyua pia, na akasema: "Sami'a llaahu liman hamidahu" Yaani: Amemsikia Mwenyezi Mungu yule aliyemuhimidi, "Rabbanaa walakal hamdu" Mola wetu Mlezi na sifa njema ni zako, na alikuwa hafanyi hivyo katika sijida.
Kutoka kwa Ubaada bin Swaamit -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume -Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Hana swala yeyote ambaye hakusoma sura kifunguzi cha kitabu (suratul faatiha)".
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliingia msikitini kisha akaingia mtu mmoja, akaswali, kisha akamsalimia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akajibu salamu, na akasema: "Rudi kaswali, kwani wewe hujaswali", akarudia kuswali kama alivyoswali mwanzo, kisha akaja, akamsalimia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Rudi kaswali kwani wewe hujaswali" (akafanya hivyo) Mara tatu, akasema: "Namuapa yule aliyekutuma kwa haki, siwezi kuswali vizuri zaidi ya hivyo, basi naomba nifundishe, akasema: "Utakaposimama katika swala basi toa takbira (sema: Allaahu Akbaru), kisha soma kiasi chepesi ulichonacho katika Qur'ani, kisha rukuu mpaka utulizane ukiwa umerukuu, kisha nyanyuka mpaka ulingane wima, kisha sujudu mpaka utulizane ukiwa umesujudu, kisha nyanyuka mpaka utulizane ukiwa umekaa, na ufanye hivyo katika swala yako yote".
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Anasimulia yakuwa yeye alikuwa akitoa takbira katika swala zote za faradhi na zinginezo, ndani ya ramadhani na nje ya ramadhani, anatoa takbira anaposimama, kisha anatoa takbira wakati anarukuu, kisha anasema: Sami'allaahu liman hamidah, kisha anasema: Rabbanaa walakal hamdu, kabla hajasujudu, kisha anasema: 'Allaahu Akbaru' wakati anapoporomoka kwenda kusujudu, kisha anatoa takbira wakati ananyanyua kichwa chake kutoka katika sijida, kisha anatoa takbira wakati anasujudu, kisha anatoa takbira wakati ananyanyua kichwa chake kutoka katika sijida, kisha anatoa takbira wakati ananyanyuka kutoka katika kikao kwenda katika rakaa ya pili, na anafanya hivyo katika rakaa zote, mpaka anamaliza swala, kisha anasema anapomaliza swala: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mimi ndiye mtu niliyekaribu zaidi kwenu nyinyi swala yangu kufanana na swala ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, bila shaka hii ndio ilikuwa swala yake mpaka alipoondoka duniani.
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao -kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu-Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - amesema: "Nimeamrishwa nisujudu kwa viungo saba, kwa paji la uso, na akaashiria kwa mkono wake katika pua yake, na mikono miwili na magoti mawili, na ncha za miguu miwili, na wala tusizikunje nguo na nywele".
Kutoka kwa Abuu Umama amesema: Alinisimulia Amru bin Abasa radhi za Allah ziwe juu yake kuwa, alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Mahala pa karibu zaidi anapokuwa Mola Mlezi na mja ni katikati ya usiku wa mwisho, ikiwa utaweza kuwa miongoni mwa wanaomtaja Mwenyezi Mungu katika wakati huo basi fanya".
Imepokelewa kutoka kwa Jariri bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Tulikuwa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akautazama mwezi usiku (yaani: Usiku wa tarehe 15) akasema: "Hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavyouona mwezi huu, hamtokingwa katika kumuona kwake, ikiwa mtaweza kufanya hima msizidiwe mkashindwa kusali kabla ya jua kuchomoza na kabla ya kuzama kwake basi fanyeni hivyo" Kisha akasoma: "Na umtukuze Mola wako kwa himdi zake njema kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuzama".
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisoma katika rakaa mbili za (sunna ya) Alfajiri {Qul yaa ayyuhal kaafiruun} na {Qul huwallaahu ahad}.