- Kupendeza kusoma sura hizi mbili baada ya suratul Fatiha katika swala ya sunna ya Alfajiri.
- Sura hizi mbili zinaitwa suratul-Ikhalswi (Utakasifu); kwa sbaabu katika suratul Kafirun kuna kujiweka mbali na yote wanayoyaabudu washirikina kinyume na Mwenyezi Mungu, nakuwa wao pia si waja wa Mwenyezi Mungu kwa sababu ushirikina wao unaporomosha matendo yao, nakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye mwenye kustahiki kuabudiwa, na ni kwa sababu katika suratul-Ikhlaswi kuna kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kutakasa matendo kwa ajili yake na kubainisha sifa zake.