- Kuificha dua ya ufunguzi wa swala, hata kama swala itakuwa ni ya kusoma kwa sauti.
- Pupa ya Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao katika kutaka kujua hali za Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika harakati zake na kutulia kwake.
- Zimekuja namna nyingine za dua ya ufunguzi, na kilicho bora kwa mtu afuatilie dua zilizokuja na kuthibiti kutoka kwake rehema na amani ziwe juu yake, ili asome hii wakati mwingine, na hii wakati mwingine.