- Nguzo hizi za swala hazidondoki kwa kusahau wala kwa ujinga, kwa dalili ya kuamrishwa mwenye kuswali kurudia, na wala hakutosheka Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kumfundisha pekee.
- Kutulia ni nguzo miongoni mwa nguzo za swala.
- Amesema Nawawi: Na hapa nikuwa atakayepunguza baadhi ya wajibu za swala basi haitoswihi swala yake.
- Amesema Nawawi: Na ndani ya hili kuna kumhurumia mwenye kujifunza na mjinga na kuwa mpole kwake, na kumuwekea wazi maswala na kufupisha makusudio, na kufupisha katika haki zake yale ya muhimu pasina yale yenye kukamilisha, ambayo yanategemea mpaka kuyahifadhi na kuyatekeleza.
- Amesema Nawawi: Na hapa nikuwa Mufti akiulizwa kuhusu jambo na kukawa na jambo jingine muhimu zaidi analolihitajia muulizaji lakini hakuliulizia basi ni sunna alieleze, na hii inakuwa ni katika nasaha na si katika kuzungumza yasiyomuhusu.
- Fadhila za kukiri mapungufu, kwa kauli yake: "Siwezi kufanya vizuri zaidi ya hivyo, basi nifundishe".
- Amesema bin Hajari: Hapa kuna kuamrisha mema na kukataza maovu, na mwenye kujifunza kumuomba mwalimu amfundishe.
- Sunna ya kutoa salamu wakati wa kukutana, na uwajibu wa kuitikia, na kwamba inapendeza kukutana mara kwa mara hata kama muda utakaribiana, na kwamba ni lazima kuitikia kwa kila mara.