Kutoka kwa Hittwan bin Abdillah Ar-Raqashi amesema: Nilisali pamoja na Abuu Mussa Al-Ash'ariy swala moja, tulipofika katika kikao (cha tahiyatu) mtu mmoja akasema: Swala imefungamanishwa na wema na zaka, akasema: Abuu Mussa alipomaliza swala na akatoa salamu, akageuka na akasema: Ni nani kati yenu aliyesema neno kadhaa wa kadhaa? Akasema: Watu wote wakanyamaza, kisha akasema: Ni nani kati yenu aliyesema neno kadhaa wa kadhaa? Watu wote wakanyamaza, akasema: Huenda ukawa ni wewe uliyesema ewe Hittwan? Akasema: Hakika niliogopa utaninyamazisha kwa neno hilo, akasema mtu mmoja katika jamaa waliokuwepo: Mimi ndiye niliyesema, na sikukusudia kwa neno hilo ila kheri, Abuu Mussa akasema: Hivi hamjui ni vipi mtasema ndani ya swala zenu? hakika Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alituhutubia na akatubainishia sunna zetu na akatufundisha swala yetu, akasema: "Pindi mtakaposwali basi nyoosheni safu zenu, kisha akuongozeni mmoja wenu, atakapotoa takbira basi toeni takbira, na anaposema: "Ghairil maghdhuubi a'laihim waladh-dhwaalliin" [Suratul Fatiha: 7], basi semeni: Aaamiin (Ewe Mola wetu Mlezi tukubalie maombi) Atakujibuni Mwenyezi Mungu, atakapotoa takbira na akarukuu basi nanyi toeni takbira na mrukuu, kwani imamu anatakiwa kurukuu kabla yenu, na anyanyuke kabla yenu", akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:"Hiyo itakwenda na ile, na akisema: Samia'llaahu liman hamidah, semeni: Allaahumma Rabbanaa lakal hamdu, Mwenyezi Mungu anakusikieni, kwani Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- alisema kupitia ulimi wa Nabii wake -Rehema na amani ziwe juu yake-: Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi, na akitoa takbira akasujudu basi sujuduni, kwani imamu anatakiwa asujudu kabla yenu na anyanyuke kabla yenu", akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hiyo inakwenda ile, na akifika mahali pa kukaa basi kauli ya mwanzo ya mmoja wenu iwe ni: Attahiyyatut twayyibaatu as swalawaatu lillaah, assalaam alaika ayyuhan nabiyyu warahmatullaahi wabarakaatuh, assalaamu alainaa wa alaa ibaadillaahis swaalihiin, ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu wa ash-hadu anna Muhammadan abduhu warasuuluhu".