- Ombi hili la kinga ni miongoni mwa dua muhimu na ni dua inayokusanya mambo mengi, kwakuwa imekusanya kuomba kinga dhidi ya shari za Duani na Akhera.
- Kuthibiti uwepo wa adhabu za kaburi nakuwa adhabu hizo ni kweli.
- Uhatari wa fitina na umuhimu wa kuomba kinga kwa Mwenyezi Mungu na kuomba dua ya kusalimika nazo.
- Kuthibitika kutokea kwa Dajali na ukubwa wa fitina zake.
- Sunna ya kusoma dua hii baada ya tashahudi ya mwisho.
- Sunna ya kuomba dua baada ya matendo mema.