- Kumebainishwa anayotakiwa kusema mwenye kusali anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu.
- Sheria ya kulingana sawa na utulivu baada ya kuinuka kutoka katika rukuu; kwa sababu haiwezekani aseme dhikiri hii ila baada ya kusimama wima na kutulia.
- Dhikiri hii ni sheria katika swala zote, sawa sawa ziwe za faradhi au za sunna.